GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,548
- 108,882
Kiongozi Mwanasiasa A
Ambaye tokea mwezi January 2018 pale ambapo Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini ( TMA ) walipotoa ‘ tahadhari ‘ ya ujio wa Mvua kubwa nchini na hasa Mkoa wa Dar es Salaam mwezi April hadi June alitumia muda wake mwingi kukutana na ‘ Wadau ‘ wa mazingira na Wataalam ili kuja na ‘ mkakati ‘ wa kuzuia ‘ mafuriko ‘ yanaloliathiri Jiji mara kwa mara na Wananchi wake ambao ni takriban 100,000 na zaidi na akafanikiwa ama kulipunguza kwa kiasi kikubwa au kulimaliza kabisa.
Kiongozi Mwanasiasa B
Ambaye tokea mwezi March katikati hadi Mwezi April amekuwa akihimiza Wanawake ‘ waliotelekezwa ‘ na Waume / Mabwana zao pamoja na Watoto wao ( ambaye wengi wao hawana uhakika kama waliopachikwa Mimba na hao Wanaume wanaowasingizia au hapana ) ambao ni takribani 3300 wamiminike / waende Ofisini Kwake ili akawapatie msaada / ufumbuzi halafu akafanikiwa tu kwa kutoa ‘ matamko ‘ ya ‘ vitisho ‘ kwa Wanaume huku kati ya Wanawake 1200 walioenda kumuona sasa hivi ‘ mafuriko ‘ haya ya Mkoani Dar es Salaam yamewaathiri sana.
Tuzo ya GENTAMYCINE kwa Kiongozi Mwanasiasa huyo ipo tayari hivyo nawasubirini nyie tu ‘ Wadau ‘ mnichagulie ni yupi inamfaa ili nikamkabidhi rasmi. Nitahesabu tu ‘Kura ‘nyingi zinamuangukia yupi hivyo atakayepata nyingi nitatafsiri ndiyo anastahili kuipata kwa mujibu wa Great Thinkers wa JamiiForums.
Nawasilisha.