Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,870
- 34,357
Kundi la 22 la manowari za jeshi la majini la China la kusindikiza meli za kibiashara liliwasili jana kwenye bandari ya Dar es Salaam, Tanzania na kuanza ziara ya siku nne nchini humo. Kwenye ziara hiyo, wanajeshi wa China wanatarajiwa kutembelea vituo vya jeshi la baharini la Tanzania na manowari za nchi hiyo, na pia watafanya shughuli mbalimbali za mawasiliano na wanajeshi wa Tanzania.
Chanzo: CRI Swahili