Kunani wizara ya afya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kunani wizara ya afya?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by double R, Apr 11, 2012.

 1. double R

  double R JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 1,356
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  Nimetafakari muda mrefu nimekosa majibu yakuridhisha kichwa changu. Hii ni baada ya kushuhudia kwa takrbani mwezi sasa(hii ni kipindi mimi nilipojua, ilianza muda mrefu), hospitali kubwa kukosa vipimo vya virusi vya ukimwi kwa kipindi chote hicho.
  Ni muda mrefu pia nilisikia kuwa vilivyoletwa vilikuwa havifai, hivyo vilikusanywa vikarudishwa.
  Sasa nashindwa kuelewa wanaogopa kuagiza vingine, vimechelewa au havina umuhimu tena?

  Kuna wananchi wengi waliopimwa na vipimo vile "fake" na mpaka sasa pengine hawaamini yale majibu, ni muda sasa hawa watu wanaishi na mashaka juu ya afya zao. Je ni wangapi wamepata shida za kunyanyapaliwa kutokana na majibu ya vipimo "fake". Hii wizara inawafikiriaje hao?
  Vipi kuhusu wafanyakazi wa afya ambao wanahatarisha maisha yao kila siku bila kujua hali za wagonjwa wanaowahudumia? Habari gani kwa mama wajawazito na watoto wao ambao wanaweza kupewa dawa kama wameambukizwa au kuzuia maambukizi kwa watoto?
  Hiyo wizara ina waziri, naibu wake katibu na wafanyakazi lukuki ambao wameshindwa kuona umuhimu wa jambo hilo. ukiwauliza sana watasema wapo kwenye mchakato? Afya za watu nazo ni mchakato. Kwa nini wanashindwa kuachia ngazi kama wameshindwa kufanya kazi? hii ni aibu sana.
  Hii serikali yetu dharula ni kifo cha mbunge au diwani wafanye uchaguzi, ila hili kwao sio dharula. Ni kweli wana bahati mambo haya hayaulizwi kwa sababu manesi wanaoona haya hawasemi wala hawalalamiki, ukosefu wa vitu kwao ni mazoea.
  Nadhani kuna wakati ifike tupate akili ya kutafakari kwa upana haya. Ndani ya miezi mitatu ni ajali ngapi zimetokea nchi hii? wangapi wamemwagikiwa damu? wangapi walistahili kujua hali zao juu ya maambukizi katika mwezi huu? Ndoa ngapi zimefungwa? wagonjwa wangapi wenye dalili za ukimwi wamehudhuria hospitali? manesi wangapi wamezalisha wanawake ambao hawakuhudhuria kliniki? watoto wangapi wamezaliwa na wanawake wasiojua hali zao za maambukizi ya virusi vya ukimwi? huduma za utoaji damu salama na upimaji hiari wa virusi vya ukimwi zimeathirikaje? Kuna walioongezewa damu kipindi cha vifaa 'fake', hawa tunawaangaliaje?

  Hebu kama serikali ina majibu ya haya iseme, nadhani ufinyu wa bajeti sio kikwazo na hata kama ni shida kuna wakati wa ajali kama ile ya meli hadi kampuni zilichangia, timu yetu ikiwa ina mechi ya kimataifa hata wabunge huchangishana hata harambee kwa ajili ya madawati zipo hadi wananchi huchangia. Wameshindwa wapi? Tunaendelea kuwa na shida nyingi kwa makosa ya wazi. Vipaumbele. Hakuna sababu ya kuendelea kuwa na viongozi wasiojali uhai wetu.
  Kama kuna taarifa ya kinachoendelea juu hili mtujuze.
   
Loading...