Kunani watanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kunani watanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kaniki1974, Mar 6, 2010.

 1. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huu upole wa watanzania, umetoka wapi? Una maana kweli kwa maendeleo ya nchi? Utatutoa kimaendeleo?

  Ukiwa mwanasiasa unaweza kuwaahidi uongo, ukawadharau na hata kuwanyanyasa na watakuangalia tu na hata kuzidi kukuchagua/kukupigia kura;

  Rais anayumbisha na kuharibu uchumi wa nchi kwa utawala mbovu usio na maono, umejaa rushwa, urafiki, kufahamiana, ufisadi, matumizi yasiyo ya lazima, yasiyozingatia vipaumbele, serikali kubwa kupita uwezo n.k na bado watamchagua kwa awamu nyingine azidi kuharibu nchi;

  Dereva katika basi anaweza kuendesha atakavyo, kutukana, kusababisha ajali, kuwashusha abiria njiani n.k lakini watanzania watakaa kimya na kuogopa kumkemea;

  Baa medi anaweza kuamua kutomrudishia mteja wake chenji au kurudisha chenji pungufu lakini mteja atamwangalia tu au kuondoka zake;

  Viongozi mbalimbali wanatukana watu hovyo, wanawanyanyasa, hawafanyi kazi ipasavyo yet, watanzania watabaki kimya na kuogopa tu;

  Makeshia katika mabenki hawafanyi kazi, wanatukana wateja, wanazembea na kusababisha mafoleni, yet wateja wapo kimya na hata kuongea kwa sauti wanaogopa!;

  Wazungu kila kukicha wanatuibia almasi Mwadui, dhahabu kule Shinyanga, Tanzanite Arusha, uranium Dodoma n.k na kunyanyasa wazawa kwa kila jinsi lakini hawapati upinzani wowote;

  Baadhi ya wawekezaji wanatukana na kunyanyasa raia hovyo hovyo tu katika mahoteli, madukani na katika biashara zao lakini hawapati upinzani wowote;

  Walimu wananyanyasa hovyo wanafunzi mashuleni na vyuoni;

  Watu wanahukumiwa vifungo vya maisha kwa sababu dhaifu/za uongo na hakuna hata wanaopinga;

  Na mengine mengi tu.

  Huu sijui upole, ujinga , ukarimu n.k UNA MAANA KWELI kwa maendeleo ya Tanzania na watu wake? Kwa nini watu hawa hawatiwi adabu na nguvu ya umma? Kwa nini blah blah hizi zinaachwa kuendelea?
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Funny we are..!
  Ni asili yetu...sidhani kama tutabadilika..
   
 3. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  So twastahili kila aina ya hujuma! God have mercy!
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Hivi besti hukufanikiwa kusoma habari ya mwizi aliyefanikiwa kuingia kwenye viunga vya IKULU ya JK na kuiba maua kibao yenye thamani ya tshs 5000, na wakati anatoka ndipo alipowasogelea askari, na kwa aibu wakamshika na kuanza kumshughulikia...Huoni kwamba we are good for nothing?
   
 5. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwi kwi kwiiiiii.... nilisikia, tusikate tamaa any way. Hope best hukubali tubaki kama hivi daima!
   
 6. a

  alibaba Senior Member

  #6
  Mar 6, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  K 1974,
  Sababu kubwa ya uoza ulioorodhesha hapo juu ni kuwa Nchi haina Utawala wa sheria. Mahakama yenyewe haijitambui inaendeshwa na wanasiasa. Angalia mfano huo wa Polisi kumpiga huyo Mwizi wa maua...........na Taasisi nyigine zote zinakwenda kimungu mungu tu. Na isiposimama sheria hakuna haki.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...