Kuna wizi mkubwa katika matumizi ya kadi ya mabasi ya mwendo kasi

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,276
Kuna wizi mkubwa katika matumizi ya hizi kadi ya mabasi ya mwendo kasi,

Kwa muda wa mwezi mmoja na nusu, nilijipa kazi ya kuchunguza ubora wa huduma ya mabasi ya mwendokasi hasa katika eneo la matumizi ya kadi za kielekitroniki, nimejiridhisha vyakutosha kwamba:

Kadi hii inamapungufu yafuatayo.

1. Ukilipia 5000, matumizi yake utasafiri mara 3 tu, Utakuwa ukikatwa marambili kuliko anayetumia risiti/tiketi ya kawaida. Yaani unalipa 1400 badala ya 650.

Kadi hii inakata pesa yako marambili yaani uki scan unapoingia na unapotoka.....

FB_IMG_1469166165968.jpg

Huenda ni ni tatizo la kiufundi ama ni wizi wa mchana kweupe....
 
Yericko upo aisee,
Inawezekana tukawatunaibiwa bila kujijua, ntaanza kuwa makini kwa kuangalia salio nishukapo.
 
Sijawai panda mwendokasi wala kutumia hyo kadi..ila kama inakata pesa mara mbili itakuwa ni tatizo la kiufundi...Mara nyingi tunaingia kwenye matumizi ya vitu ambavo hatujajiandaa au kuweka mfumo mzuri wa matumizi yake au hautujaiandaa vizuri kukabiliana na changamoto zake..
 
Kuna wizi mkubwa katika matumizi ya hizi kadi ya mabasi ya mwendo kasi,

Kadi hii inamapungufu yafuatayo.

1. Ukilipia 5000, matumizi yake utakuwa ukikatwa marambili kuliko anayetumia risiti/tiketi ya kawaida. Yaani unalipa 1400 badala ya 650.

Kadi hii inakata pesa yako marambili yaani uki scan unapoingia na unapotoka.....

View attachment 369314

Huenda ni ni tatizo la kiufundi ama ni wizi wa mchana kweupe....
NI KWELI YAKATA MARA 2..HUU NI WIZI WA NCHANA KWEUPE.
 
Ngoja nikaangalie salio. Nimenunua kadi hio na nimesafiria mara mbili. Yaani kwenda na kurudi safari mbili. Kwa hesabu sahihi natakiwa nitumie tzs 2,600. Salio inabidi liwe 1,900. Nitaleta mrejesho.
 
Sijawai panda mwendokasi wala kutumia hyo kadi..ila kama inakata pesa mara mbili itakuwa ni tatizo la kiufundi...Mara nyingi tunaingia kwenye matumizi ya vitu ambavo hatujajiandaa au kuweka mfumo mzuri wa matumizi yake au hautujaiandaa vizuri kukabiliana na changamoto zake..
Kama ni tatizo la kiufundi ni kwa nini isikate pesa pungufu?

Huu ni wizi tu sawa na makampuni ya simu yanavyoibia wateja wake wala tusilete visingizio.
 
Kuna wizi mkubwa katika matumizi ya hizi kadi ya mabasi ya mwendo kasi,

Kwa muda wa mwezi mmoja na nusu, nilijipa kazi ya kuchunguza ubora wa huduma ya mabasi ya mwendokasi hasa katika eneo la matumizi ya kadi za kielekitroniki, nimejiridhisha vyakutosha kwamba:

Kadi hii inamapungufu yafuatayo.

1. Ukilipia 5000, matumizi yake utakuwa ukikatwa marambili kuliko anayetumia risiti/tiketi ya kawaida. Yaani unalipa 1400 badala ya 650.

Kadi hii inakata pesa yako marambili yaani uki scan unapoingia na unapotoka.....

View attachment 369314

Huenda ni ni tatizo la kiufundi ama ni wizi wa mchana kweupe....
Kuna jamaa ameniambia kwamba asipotajirika ndani ya miezi 6 anarudi kijijini .
 
Sidhani kama inakata mara mbili,mimi kila siku huwa napanda hizi gari,juma tatu hadi juma mosi..Niki load elfu 5 huwa na scan mara 6,yani juma 3 hadi juma mosi...Kama wanaiba inawezekana labda but sio kwa kiwango cha double deduction..
 
Kwanza nakupongeza sana SIRCHIEF,
MM NIMELALAMIKA SAANA JUU YA WIZI UNAOFANYA NA DART, watu walinipinga niligundua kua kuna wizi kwa kua nil ilia elf 5000 LAKINI nimetumia kwa Safari 3 TU one way.
Naomba vyombo husika viingilie kati WIZI wa aina hii, na baada ya kuona wanafaidika na huu mpango wanatangaza kua matumizi ya tiketi mwisho mwezi july 2016 hii ni Kosa kubwa
 
nilipata Bahati ya kuongdea na mfanyakazi mmoja shem wangu akasema hivi "card ziko sensitive sana unatakiwa ufanye single scan ukijichanganya TU wanakata mara moja zaidi,akasema watu wanalakamika kweli ,tofauti na zile karatasi unaweza ukascan zaidi ya mara moja zina delay hivi" nahisi mnakosea kwa kufanya dubble scaning kwa Bahati mbaya

nijuavyo nchi za watu kama train unascan kudetect wapi umepanda kwa distance utakayo safari ukiteremka ndio wanakata
naweza kurekebishwa
 
Sijabahatika kupanda ma bus lakini Dunia ya wapi un scan ticket wakati wa kutoka? Huu wizi mkubwa sana.
Yaani wanakera hadi basi. Usiposcan unapotoka hayo machuma hayafungiki utoke.Halafu Ubungo Shekilango wamefunga mlango mmoja, unatembea umbalimrefu kufuata mwendo kasi. Alama ya Zebra zimefutika kariakoo msimbazi.
 
Back
Top Bottom