Kuna watu walizoea kubebwa!

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
13,221
14,417
Awamu hii naomba nikiri kabisa ni awamu ya kusomesha watu namba kama ilivyokuwa kwenye wimbo wa hawa jamaa! Kwanza wanaosemeshwa namba ni maccm yaliyoshinda majimboni, haya majamaa yalikuwa yanapiga kampeni huku mitaani eti oooh nipeni kura ili mpate waziri (hawa wote chali). Sasa hivi watakuja mitaani kwa kujificha. Rais aliwaona hawafai ndo maana kaenda kuazima nje kwa baadhi ya wizara. Yaani Kangi Lugola hata wizara ya wanyamapori ulikuwa hufai? Masele hata ujenzi hukufit? Wacha muisome namba!

Kundi la pili ni wale waliotegemea kubebwa kwa mgongo wa udini! Awamu iliyopita ilikuwa ya kupalilia udini sana lakini awamu hii haiangalii mambo ya udini hata kama itakuwa 2/10 ni sawa tu mradi watu wawe na uwezo. Katika kuthibitisha hilo baraza hili ni 9/22 sasa sijui waliozoea kubebwa wataandana? Wacha tusubiri, time will tell!! "HAPA KAZI TU" Usitegemee dini itakubeba au jinsi itakubeba!
 
inauma sana mtu alikuwa waziri then anaachwa wizala inakaa wazi siku kadhaaa kutafuta mrithi wakati aliyekuwepo ni mbunge..kweli wataisoma no
 
Huyu Mama Dr. Asha Rose Migiro naona kapotea haonekani tangu mchakato wa pale Dodoma simsikii tena. Vipi au ndo kastaafu na yeye siasa?
 
Bado wanasubiri kupata mgao wa vyeo, wanasubiri mshikaji wao amalize kufanyiwa massage kwa kuru a kitita ha hela zetu
 
Waache wasubiri, tutawabeba sisi na kuwabwaga majumbani kwao, wengine wachumba wao wamekumbwa na kipindupindo kalagabaho
 
Awamu hii naomba nikiri kabisa ni awamu ya kusomesha watu namba kama ilivyokuwa kwenye wimbo wa hawa jamaa! Kwanza wanaosemeshwa namba ni maccm yaliyoshinda majimboni, haya majamaa yalikuwa yanapiga kampeni huku mitaani eti oooh nipeni kura ili mpate waziri (hawa wote chali). Sasa hivi watakuja mitaani kwa kujificha. Rais aliwaona hawafai ndo maana kaenda kuazima nje kwa baadhi ya wizara. Yaani Kangi Lugola hata wizara ya wanyamapori ulikuwa hufai? Masele hata ujenzi hukufit? Wacha muisome namba!

Kundi la pili ni wale waliotegemea kubebwa kwa mgongo wa udini! Awamu iliyopita ilikuwa ya kupalilia udini sana lakini awamu hii haiangalii mambo ya udini hata kama itakuwa 2/10 ni sawa tu mradi watu wawe na uwezo. Katika kuthibitisha hilo baraza hili ni 9/22 sasa sijui waliozoea kubebwa wataandana? Wacha tusubiri, time will tell!! "HAPA KAZI TU" Usitegemee dini itakubeba au jinsi itakubeba!
Wagalatia hamuishi vituko, haya mumpe na uenye heri kabisa,
 
Hata huyo Nape na Makamba wakileta u CCM CCM wataisoma namba, wako chini ya uangalizi tu hao, Hapa ni kazi tu hatuangalii ukada. Vile vikina mama vilivyozoea kupewa tu vyeo kwasababu tu ya jinsia bila kuangalia sifa za utendaji nao hao byebye, mambo ya 50 - 50 bila tija hapa kazi tu hatuna hiyo nafasi. Wale wafunga gidamu za wakubwa nao byebye, Sisi Hapa Kazi tu tunavaa buti za kuchomekea tu. Wale waliopata vyeo kwa ukuadi wa kutafutia wakubwa videmu byebye! Hapa Kazi tu hatuna muda wa massage! Wale sampuli ya Benson Bana wanaosifia kila jambo ama la chama tawala au la mkuu wa nchi hata kama linakiuka katiba na kwenda kinyume na haki za binadamu, na maranyingi hawana msimamo thabiti kwa jambo fulani, wanaobadilika badilika kama kinyonga nao hao byebye! Duh hadi raha!
 
Dr. Mary Michael Nagu

Huyu naye yuko anaisoma namba taratibu! Dr. Kamala kwishney, Mh. Chegeni finito! Lazaro Nyarandu kuishney! Wakuu let us be honest, hivi mtu unaacha Ubalozi unakinbilia ubunge maanake nini? Au ndo hao wanaoota uwaziri ili wapige mpunga kisawasawa? Hivi heshima ya mbunge inazidi ya balozi? Kwa kweli Dr. Kamala atakuwa anajuta sana (kutoka Belgium mpaka Nkenge?).
 
Ubalozi hauna fedha ndefu. Unaishi kwa bajeti finyu tuu na pesa ya madurufu ya visa na kama ndio umepangiwa msumbiji au burundi imekula kwako labda uwe smuggler
 
Back
Top Bottom