Kuna watu si wastaarabu kwenye usafiri wa umma, tumepanda na mzee wa makamo anaropoka taarifa za watu ovyo

Kuna watu si wastaarabu kwenye usafiri wa umma, tumepanda na mzee wa makamo anaropoka taarifa za watu ovyo

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,160
Reaction score
11,228
Kwa kweli kuna watu hawana ustaarabu kabisa. Unawezaje kuzungumzia maisha ya watu wengine hadharani, bila hata kujali faragha yao, tena ukiwa kwenye usafiri wa umma? Hujui hata kama mmoja wa abiria ni ndugu au jamaa wa huyo unayemzungumzia.

Tulipanda basi pale Segerea na kulikuwa na mzee wa makamo ambaye alipigiwa simu, nadhani na rafiki yake wa zamani waliowahi kushirikiana katika harakati za maisha. Kuanzia Tabata Segerea hadi Mwananchi, alikuwa anaongea kwa sauti kubwa kiasi kwamba kila abiria alilazimika kusikiliza, wengi wakibaki kushangaa na kusikitika.

Cha kushangaza zaidi, mazungumzo yake yalihusu maisha binafsi yake na ya marafiki zao wengine. Alimtaja mtu kwa jina la Frank fulani, akaanza kuelezea maisha yake ya sasa, mahusiano yake, hali yake ya kiafya, hadi historia ya mzazi wake aliyewahi kufanya kazi serikalini, pamoja na maisha aliyokuwa nayo zamani. Kwa maelezo aliyotoa, mtu angeweza kabisa kumtambua huyo Frank kama angeamua kufuatilia.

Kwa kweli nachukia sana tabia ya watu kuongea kwa sauti kubwa kwenye usafiri wa umma bila kujali faragha za wengine.

Pia soma Jinsi ya Kuzuia watu kuchungulia, kusoma au kuona unachofanya kwenye simu yako ukiwa kwenye usafiri wa umma
 
Back
Top Bottom