Kuna watu hufikiria sana bila kutumia hisia na wengine huhisi sana bila kutumia akili

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
395
Shida kubwa ya wanadamu ni kwamba wengine hufikiria sana bila kutumia hisia na wengine huhisi sana bila kutumia akili.

Aghalabu wale wote wanaofikiri sana bila kutumia hisia hao mambo yao hukosa utu, na wale ambao huwa wanahisi sana bila kutumia akili hao mambo yao hukosa maarifa.

Unajua ni lazima tufahamu wapi pa kuusikiliza moyo na wapi pa kuusikiliza ubongo. Ikiwa utachanganya matumizi ya vitu hivi viwili basi utaishia kuogelea kwenye mto wa machozi yako mwenyewe.

Usiamini kila unachokifikiri, ila jitahidi kufikiri kila unachokiamini. Kama wewe ni muungwana basi ni lazima ufahamu tamaa na majuto haviachani, hivyo panapohitajika akili ukitumia hisia basi umeenda na maji.

Labda nikwambie tu, wapo baadhi ya watu wanaojutia maisha yao kwa kuitikia NDIO mapema sana, na wengine wanaojutia maisha yao kwa kuitikia HAPANA wakiwa wamechelewa mno.

Sio tu jibu sahihi lijibiwe kwa wakati sahihi bali hata mbele ya mtu sahihi. Hapa naongelea 'Utatu Sahihi' yaani JAMBO sahihi ndani ya WAKATI sahihi mbele ya MTU sahihi.

Ikiwa utachanganya kimoja basi kuna uwezekano wa kuvitofoa vingine, na ndio maana vipo vingi vya halali ambavyo hugeuka kuwa batili ikiwa tu vitachelewa kutekelezwa.

Najua unaweza ukawa hujanielewa nilichoandika, ila ni haki yangu mimi mwandishi kuchagua aina ya lugha kufikisha ujumbe. Kabla hujapuuza uumbe huu, basi fahamu kwamba ni ujumbe sahihi, kwako mtu sahihi, ndani ya wakati huu sahihi.

Ahsante kwa kunisikiliza, kwenye kalamu ni yule yule kijana wenu wa kila siku Amani Dimile
1693261714322.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom