Kuna watu hufanya mapenzi yachukiwe

Kuna watu hufanya mapenzi yachukiwe

Unajikuta unaanza kumpenda mtu, taratibu mnaanza ukaribu. Unamchukulia kama ni mtu special kwako. Unampa attention yote.
.
Mnafanya mengi ya kukumbukwa, maisha ya mahusiano unaona matamu. Kwake unaona ndio umetua mzigo.
.
Lakini, katikati ya safari mambo yanaanza kubadilika.
.
Mawasiliano yanapungua, uaminifu unapotea na mapenzi yanapoa. Masikini, unajitahidi kwa hali na mali kurudisha mapenzi, unajitahidi ku-fix mambo yasiharibike, unaweka jitihada kuokoa mapenzi lakini jitihada ni zako peke yako, mwenzako yuko mbali.
.
Unachoka na kukata tamaa. Unalia kila siku iitwayo leo, huna raha, moyo unauma, akili imesimama, chakula hakipandi. Vidonda vya tumbo vimechachamaa.
.
Unatamani umsahau lakini akili na moyo unagoma kabisa.
.
Unatakiwa uelewe hili, toka mwanzo yale hayakuwa mapenzi. Ilikuwa ni infatuation. Tena shukuru umejua mapema. Kwa sababu Mwenye upendo huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai, wala hajivuni.
.
Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya, hafurahii uovu, bali hufurahia ukweli. Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote. Upendo hauna kikomo kamwe.
.
Kubaliana na hali, kuteleza sio kuanguka. Ipo siku utapata mtu atakaekupenda kweli na hapo ndipo utakapoamini kuwa kuna watu wanajua kupenda.
.
GOD BLESS YOU!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ujumbe mzuri sana mkuu,

Haya mapenzi bwana unaweza kujikuta umempenda mtu kumbe siyo chaguo lako. Anakutenda na kukufanyia mabaya ya kila aina. Ila kumbe hayo yanakuwa kama darasa au daraja la kukuvusha kuelekea kwa mtu sahihi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
yani mwanaume mzima unalia kuachwa hawa madem waliojaa mtaani visu namna hio afu unalia lia.... mkishauriwa mtafute michepuko mara ooh ukimwi ooh sijui huyu nampenda..... sasa angalia unalia lia kama mtoto wa kike michepuko ina umuhimu sana kwenye kizazi chetu

W, G, S na D popote mlipo michepuko yangu mnasaidia sana hamjui tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Bado hujapenda mkuu siku ukiwa ktk season ya mapenz halisi huu ujumbe utakuja kuurudia kusoma..... Kila kheri ktk michepuko yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujumbe mzuri sana mkuu,

Haya mapenzi bwana unaweza kujikuta umempenda mtu kumbe siyo chaguo lako. Anakutenda na kukufanyia mabaya ya kila aina. Ila kumbe hayo yanakuwa kama darasa au daraja la kukuvusha kuelekea kwa mtu sahihi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ofcoz wanasema huwezi jua kidole kirefu km kifupi hakipo ndivyo ilivyo kwenye mapenzi ili kumpata mtu sahihi kwako lazima ukutane na mtu ambae atauumiza moyo wako na kuuponda ponda zaid

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajikuta unaanza kumpenda mtu, taratibu mnaanza ukaribu. Unamchukulia kama ni mtu special kwako. Unampa attention yote.
.
Mnafanya mengi ya kukumbukwa, maisha ya mahusiano unaona matamu. Kwake unaona ndio umetua mzigo.
.
Lakini, katikati ya safari mambo yanaanza kubadilika.
.
Mawasiliano yanapungua, uaminifu unapotea na mapenzi yanapoa. Masikini, unajitahidi kwa hali na mali kurudisha mapenzi, unajitahidi ku-fix mambo yasiharibike, unaweka jitihada kuokoa mapenzi lakini jitihada ni zako peke yako, mwenzako yuko mbali.
.
Unachoka na kukata tamaa. Unalia kila siku iitwayo leo, huna raha, moyo unauma, akili imesimama, chakula hakipandi. Vidonda vya tumbo vimechachamaa.
.
Unatamani umsahau lakini akili na moyo unagoma kabisa.
.
Unatakiwa uelewe hili, toka mwanzo yale hayakuwa mapenzi. Ilikuwa ni infatuation. Tena shukuru umejua mapema. Kwa sababu Mwenye upendo huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai, wala hajivuni.
.
Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya, hafurahii uovu, bali hufurahia ukweli. Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote. Upendo hauna kikomo kamwe.
.
Kubaliana na hali, kuteleza sio kuanguka. Ipo siku utapata mtu atakaekupenda kweli na hapo ndipo utakapoamini kuwa kuna watu wanajua kupenda.
.
GOD BLESS YOU!

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona maumivu kila kona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utapata tu wakufanana naye,mapenzi hutakiwi kulazimisha,hujawahi kuona umempenda mtu akatokea mwingine mzuri zaidi yake na ukatamani umtongoz?watoto wazuri bado wapo imarisha uchumi wako uanze kuwatafuna.
 
Hahahaha kiukweli huu ujumbe leo nimeamua tu kuutoa km kuwakumbusha wahanga km mie ambao niliupitia hapo awali sio sasa mkuu...... But ushaur wako ni mzuri ofcoz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom