Chrix_Tz
JF-Expert Member
- Apr 15, 2015
- 880
- 1,101
Unajikuta unaanza kumpenda mtu, taratibu mnaanza ukaribu. Unamchukulia kama ni mtu special kwako. Unampa attention yote.
.
Mnafanya mengi ya kukumbukwa, maisha ya mahusiano unaona matamu. Kwake unaona ndio umetua mzigo.
.
Lakini, katikati ya safari mambo yanaanza kubadilika.
.
Mawasiliano yanapungua, uaminifu unapotea na mapenzi yanapoa. Masikini, unajitahidi kwa hali na mali kurudisha mapenzi, unajitahidi ku-fix mambo yasiharibike, unaweka jitihada kuokoa mapenzi lakini jitihada ni zako peke yako, mwenzako yuko mbali.
.
Unachoka na kukata tamaa. Unalia kila siku iitwayo leo, huna raha, moyo unauma, akili imesimama, chakula hakipandi. Vidonda vya tumbo vimechachamaa.
.
Unatamani umsahau lakini akili na moyo unagoma kabisa.
.
Unatakiwa uelewe hili, toka mwanzo yale hayakuwa mapenzi. Ilikuwa ni infatuation. Tena shukuru umejua mapema. Kwa sababu Mwenye upendo huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai, wala hajivuni.
.
Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya, hafurahii uovu, bali hufurahia ukweli. Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote. Upendo hauna kikomo kamwe.
.
Kubaliana na hali, kuteleza sio kuanguka. Ipo siku utapata mtu atakaekupenda kweli na hapo ndipo utakapoamini kuwa kuna watu wanajua kupenda.
.
GOD BLESS YOU!
Sent using Jamii Forums mobile app

Kazi sana hasa sie wenye mapenzi ya kweli tunakosa kabisa imani siku hizi.... 