Ulongupanjala
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 8,508
- 13,974
Habari za Jumapili?
Wengi wetu tumewahi kuona na kusikia matukio mbalimbali ya FUMANIZI zikitokea katika maeneo ya ya bar,guest house/hotel nk lakini wiki chache zilizopita ilitokea funga kazi ya FUMANIZI.
Stori iko hivi:
Jamaa alikuwa anaishi na mke wake kwenye nyumba ya ghorofa mitaa fulani hapa Arusha,kwa kuwa jamaa anafanya kazi za kusafiri mara kwa mara mke wake alichukua nafasi hiyo kuleta mwanaume mwingine ndani ya nyumba ya mume wake na kumruhusu kulala katika kitanda cha mumewe na kuvunja amri ya sita huku akiwa amepaki gari yake,kwa kifupi jamaa alikuwa anakuja na kulala na kuvunja amri ya sita kama vile yeye ndi baba mwenye nyumba halali.
Siku ya tukio jamaa alikuwa amesafiri na yupo mbugani,akapata taarifa kuwa jamaa ameshaingia kwenye chumba chake na game linapigwa,jamaa aliwasha gari usiku wa manane na kufika na kupaki gari yake jirani na nyumba yake na kuendea na kugonga geti lake kimya kimya mara baada ya mlinzi wa kimasai kufungua alikula vibao kadhaa na kuamrishwa aende kuwagongea mke wake na kuwadanganya kuwa kuna dharula,alipoenda kugonga jamaa anayekula mke wa mtu akatoka chumbani huku kajifunga taulo la jamaa na kushuka ngazi,baada ya kushuka ngazi kadhaa jamaa akashtuka kuwa sio kawaida kutakuwa na kitu cha ziada akarudi mbio chumbani,mwenye mke/nyumba kuona hivyo naye akatoka alipojificha na kuanza kumkimbiza jamaa kuelekea chumbani.
Ile kufika chumbani jamaa anayeiba mke wa mtu aliwahi kufunga mlango,kutotokea bonge la vurugu na hatimaye mlango kuvunjwa huku majirani wakijitokeza kutoa msaada wa kuwaamulia ugomvi wao,huku kila mmoja akijihami mwenzie asije kutumia silaha.
Mwisho, mke alitolewa vitu vyake nje hasa mavazi na kuamliwa kuondoka usiku huo huo pamoja na mchepuko wake.
Jamaa mwenye nyumba alichukua watoto wake wadogo na kuwapeleka nyumbani kwa mama yake mzazi ili awalee na alifunga nyumba yake na kuweka mlinzi mpya,maana yule wa kimasai alitokomea kusiko julikana baada ya kuona naye atatiwa hatiani kwa kuto ripoti juu ya mchepuko aliyekuwa anakuja kulala na mke wa jamaa mwenye nyumba.
My take: Hivi baadi ya wanawake wakoje mpaka kuwa na uthubutu wa kuleta mchepuko kwenye nyumba ya mumuwe tena na kuvunja amri ya sita kwenye kitanda cha mumuwe?
Mwanamke alipendwa sana na jamaa na kupata mahitaji yote muhimu mpaka gari ya kisasa ya kutembelea alinunuliwa,japokuwa mwanamke alikuwa mama wa nyumbani.
Leo hii mwanamke aliyekuwa anaishi kwenye nyumba ya kisasa ya ghorofa ametokomea kusiko julikana hata familia yake na ndugu zake hawamjui aliko hali kadhalika simu alinyang'anywa na mume wake siku ya fumanizi,ili kuficha aibu yake.
UKITAKA KUISHI MAISHA YA AMANI NA FURAHA ACHA KABISA MICHEPUKO,IPO SIKU UTAJUTA.