Kuna wanaCCM wanataka kunichafua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna wanaCCM wanataka kunichafua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Feedback, Jul 13, 2011.

 1. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  'Wanashirikiana na baadhi ya vyombo vya habari'

  KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (NEC), Nape Nnauye, amefichua mkakati mzito wa kumchafua, unaodaiwa kufanywa na wapinzani wake kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Alisema mkakati huo unafanywa na watu wasioitakia mema CCM, wakiwemo baadhi ya wanasiasa kwa kutumia baadhi ya vyombo vya habari.

  “Wameanza kutumia baadhi ya vyombo vya habari kutoa taarifa za kupika (cooked stories) ambazo zimeshaanza kutekelezwa kwa lengo la kukidhi matakwa na masilahi yao yakiwemo ya kuwagombanisha viongozi, wanachama na umma kwa ujumla,” alisema Nape.

  Ingawa hakuwa tayari kutaja vyombo vya habari alivyodai vimeandaliwa kumchafua yeye, Rais Jakaya Kikwete na wengine, Nape alisema baadhi ya taarifa hizo za uzushi zitaanza kuonekana leo.


  Nape Nape Nape............usianze kutafuta mchawi mchana kweupe, usiwasingizie wana CCM mchawi ni maneno yako ukiwemo uongo wa kuwapa siku 90 wanachama ulowakuta sasa yanaanza kukurudi.


  Source: Tanzania Daima na Clouds FM
   
Loading...