Weston Songoro
JF-Expert Member
- Feb 17, 2014
- 2,793
- 1,083
Naona uanachama wa Wema Sepetu ukiyeyuka ndani ya CHADEMA. Sijajua hii movie itaishia wapi ila wakati ndio utaamua.
1. Yametokea mabishano makali baina ya Upande wa Wema Sepetu na Wawakilishi wa CHADEMA chini ya Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya na Mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu. Lissu anatumika kumshawishi Wema kwa vile wanatoka mkoa mmoja. Esther Bulaya anatumika kwa sababu wana mahusiano ya muda mrefu. Hata hivyo. Mabishano yaliyoanza tangu jana asubuhi ambayo yalishindwa kufikiwa muafaka nyumbani kwa Freeman Mbowe, Reef Appartment, Mikocheni yameendelea usiku kucha hadi leo asubuhi. Mpango ulikuwa Wema Sepetu atangaze kujiunga na CHADEMA jana jioni. Hata hivyo, kwa kuwa walikuwa hawajafikia makubaliano, Press Conference ambayo ilitangazwa na Msemaji wa CHADEMA, Tumaini Makene ilishindikana kufanyika
Upande wa Wema Sepetu ukiongozwa na Mama yake Mzazi ambaye anapata shinikizo la Steven Nyerere unasisitiza kuwa ili wema Sepetu ajiunge na CHADEMA, chama hicho kiandae kitita cha shilingi milioni 300. Hoja wanazotoa ni kwamba, Wema ana Wafuasi wengi ambao wanaamini watamfuata CHADEMA. Pili wanasema kuwa Wema anajitoa mhanga na hivyo kuyaweka maisha yake rehani. Tatu wanasema kwa sasa Wema Sepetu ameharibiwa hadhi yake baada ya kutajwa kuhusika na matumizi ya madawa ya kulevya hivyo kuna uwezekano shughuli zake zikaathirika. Hivyo ili aweze kuwa mwanachama wa CHADEMA bila kuwa na stress za maisha, wanataka kiasi hicho ili kuboost maisha yake.
CHADEMA wanasisitiza kuwa watampa shilingi milioni 150 hasa kutokana na ukweli kuwa wameshatumia fedha nyingi tangu mwaka 2015 iliposhindikana msanii huyo kujiunga CHADEMA.
2. Wema hana mgogoro na CCM bali ana ugomvi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Baadhi ya wana CCM walio karibu na Wema Sepetu akiwemo Nape Nnauye na Mwigulu Nchemba wanajitahidi kumuweka sawa Wema na kumwambia kuwa ugomvi wake na Makonda usisababishe kuhama chama. Kwani hata huko CHADEMA anakoelekea kuna watu atagombana nao.
3. CHADEMA wanamhitaji zaidi Wema kuliko Wema anavyoihitaji CHADEMA. Kwa sasa inaonekana dhahiri kwamba ni CHADEMA ndio wanaohangaika kuhakikisha kuwa Wema anaenda CHADEMA. Kampeni kubwa inafanywa pia kupitia mitandao ya kijamii hususan Instagram. CHADEMA wanamtumia Mange Kimambi kumshawishi Wema Sepetu kwa ahadi kuwa atapewa Ubunge wa Viti Maalum mwaka 2020.
4. Kuvuja kwa Voice Note. Voice Note iliyovunja ya Steven Nyerere na Mama yake Wema Sepetu wakipanga namna ya kuiibia fedha CCM imeharibu kila kitu. Inaonekana baadhi ya wazee wa CHADEMA wameanza kushtuka kuwa huenda ujio wa Wema Sepetu ni mkakati ulioandaliwa kwa malengo ya kiuchumi zaidi.
5. Kurejea kwa baadhi ya wasanii CCM. Historia inaonesha kuwa baadhi ya wasanii wa kike hawadumu upinzani wanapohama CCM. Alichofanya Jacquiline Wolper mwaka 2015 inawapa somo CHADEMA kuwa hata Wema atarejea katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020.
6. Wema Sepetu kukataa kukabidhi kadi ya CCM kwa viongozi wa CHADEMA. CHADEMA walitoa masharti kwamba, ili waamini kuwa watakuwa naye muda wote, awakabidhi kadi yake ya CCM ama aichome moto huku akijirekodi na video yake kuweka kwenye ukurasa wake wa Instagram kama alivyofanya Mange Kimambi. Hata hivyo, yaelekea Wema Sepetu hakubaliani na hoja hiyo kwani anaamini kufanya hivyo hakutakuwa na tija kwake mbele ya safari.
Je Wema anaenda ama haendi CHADEMA? Wakati utaamua.