Kuna uwezekano wa Hard Disk Drive kuwa External Drive

Kuna uwezekano wa Hard Disk Drive kuwa External Drive

Corner stone

Member
Joined
Jan 3, 2020
Posts
32
Reaction score
41
Habari ya wakati huu wana JF,

kwenu wabobezi wa tehama, kuna uwezekano wa kuifanya hard disk ya 4TB ikawa external. Na nini vya kuzingatia wakati wa kufanya mchakato huo wa mabadiliko.

Natanguliza shukrani
 
Ichukue hiyo HDD zunguka nayo kwenye maduka ya PC tafuta external enclosure inayofit kisha ijaribu kwenye hiyo enclosure ikikaa tayari una external
 
Hiyo hdd ni ya laptop au desktop.

Inawezekana tena kama ni ya laptop ni rahisi zaidi case zake zinauzwa 10000- 15000 tu.
 
inawezekana kabisa hiyo mzee
 
Chunguza kwanza kama connection yake ni PATA au SATA.
 
hiyo adapter unatakiwa kuinunua pia?
Screenshot_20230501-194026.jpg
 
Habari ya wakati huu wana JF,

kwenu wabobezi wa tehama, kuna uwezekano wa kuifanya hard disk ya 4TB ikawa external. Na nini vya kuzingatia wakati wa kufanya mchakato huo wa mabadiliko.

Natanguliza shukrani
Ni swala dogo kama kunywa maji chukua hiyo Internal Hard disk yako nenda kwenye duka la vifaa vya computer mwambie akupatie external case ya hard disk then chagua inayofit then itakuwa imeisha hiyo
 
Back
Top Bottom