Kuna uwezekano mkubwa tukawa na raisi wa nchi ambaye ni rafiki kipenzi wa majambazi!
Ni jambo linaloonekana la hatari, haliwezekani kutokea lakini kama ukifuatilia kwa makini kampeni zinazoendelea hivi sasa napata mashaka uwezekano huo kwa sasa unazidi kuongezeka. Hebu tufuatilie kwa makini kauli au matendo haya na tuone uhatarishi huo unakujaje?
Kwa taswira hii naogopa yawezekana siku akaingia kiongozi atakayeona huitaji wa kuwa na kundi la maharamia, je tutaipeleka wapi nchi yetu? ni kweli Tanzania hii inaweza kuendeshwa bila ya kufuata taratibu?
Najua wengi wetu walikuwa wakidhani amani tuliyonayo leo imekuja kwa bahati nasibu, hawaoni kuwa kuna haja ya viongozi kuandaa mikakati thabiti ya kuilinda na kudumisha amani yetu kwa kufuata sheria na taratibu tena sote tusimamie kwa nguvu zetu zote!
Naomba niige kibwagizo cha Ally Choki (ukiwaunaona elimu ni ghali basi jaribu ujinga) na wewe ukiona amani ni ghali basi chagua viongozi wa aina hizo nilizotaja hapo juu.
Ni jambo linaloonekana la hatari, haliwezekani kutokea lakini kama ukifuatilia kwa makini kampeni zinazoendelea hivi sasa napata mashaka uwezekano huo kwa sasa unazidi kuongezeka. Hebu tufuatilie kwa makini kauli au matendo haya na tuone uhatarishi huo unakujaje?
- kuhamasisha vijana wasitii mamlaka
- Kuna baadhi ya vijana wanahamasishwa wasitii mamlaka tu kwa ajili ya kulinda haki. Viongozi wa vyama fulani wanaamini kuwa wananchi bila ya kuwa na utaratibu wanaweza kuisimamia haki wao wenyewe. vijana wanaweza kuwa wasimamizi wa haki na waamuzi ambapo wataona haki zao zinapuuziwa. kwa bahati mbaya wanaopewa nafasi hii adimu ya maamuzi hawajui mipaka ya haki zao, kuna kila ushahidi kuwa sehemu nyingi wamekuwa wakivunja sheria, lakini miongoni mwa watu au mamlaka wanazoaminishwa kuwa hazifai ni askari, jeshi la wananchi, usalama wa taifa na tume za uchaguzi na serikali kuu. katika hali hii tutarajie vurugu ambazo kwa sehemu kubwa watoa kauli wanajua hawatohusika moja kwa moja. tumtolee mfano Mtu kama Mnyika hatokuwepo ktk kituo chochote kulinda kura ingawa ni kijana, lakini anaweza hamasisha vijana kusimama ktk vituo. Hapa napata mashaka na viongozi wetu ambao wanataka kuchukua dola lkn hawawezi hata kuheshimu taratibu kuu za kuingia ktk dola.
- kuingilia uhuru wa mahakama
- Miongoni mwa kauli za maraisi zinaingilia uhuru wa mahakama na wametamka wazi kuwa watatengua maamuzi hayo na kuwaachia baadhi ya watuhumiwa na wafungwa wa kesi mbalimbali. maamuzi haya yanaweza kuchekelewa na baadhi ya watu hasa waharifu lakini kwa wale walioumizwa na uharifu huo ni kuwatamanisha eiza walipe kisasi au wachukue hatua nyingine.tuchulie mifano ya kuachiwa kwa watuhumiwa wa uharifu Zanzibar bila ya kufuata taratibu, kunaweza kuhamsha hisia na machungu makali kwa waumini ambao nyumba zao za ibada ziliumizwa na uharifu au viongozi wao walikumbwa na kadhia kadhaa za uharibifu huo.tunaweza kuwarekebisha wagombea wenye kauli hizi kwa kuwaomba wahimize haki zitende na mifumo husika ihamasishwe kufanya review ya case zenye utata na kuona kama kuna uwezekano wa kuzirejesha mahakamani, kuharakisha ushahidi na kuongeza speed ili hukumu ziende haraka na zizingatie haki pande zote.
- Urafiki na baadhi ya makundi hatarishi katika jamii.
- kuna baadhi ya wagombea wanadai kuwa na urafiki na baadhi ya makundi ktk jamii. Si lazima ikamaanisha kuwa kundi lote ni hatarishi lakini ukijinasibu na kundi fulani lazima ulinyambulishe vya kutosha ili uondoe mashaka yoyote yanaweza kutokea sijui kama ndio sehemu ya kuleta hamasa ktk uchaguzi au ni kweli wanaamini katika hilo. Mfano baadhi ya wagombea wanasema kuwa na urafiki na watu wa bodaboda. Wengi wetu tunawaheshimu, either sisi wenyewe, au tuna vijana wetu, rafiki zetu au ndugu zetu miongoni mwa makundi haya ya vijana. wengi ya vijana wa bodaboda ni salama na wema ktk jamii, lkn ikumbukwe kuwa wapo ambao hawafai kutokana na matukio. ningependa ujiulize kama huyu rafiki anaamini katika kutokuwepo kwa mipaka na taratibu kwa kundi hili ndio urafiki? naona kama anawaeleza kuwa ataondoa taratibu zote zilizowekwa na kuwafanya rafiki hawa kukosa raha. Lakini hapa ndipo kwenye shida zaidi. Kwa sasa katika hili kundi kuna watu wengi zaidi wanaokamatwa kwa kujihusisha na vitendo vya uharifu, au wanaofanikiwa kufanya uharifu na kutoroka. Katika kila matukio 10 ya ujambazi mjini, basi angalau 1 muhusika atafanya akiwa na bodaboda, najiuliza tu na hawa ni miongoni mwa marafiki wa raisi? katika uharifu mdogo wa uporaji wa simu, vipochi na mabegi ya laptop kwa jiji la Dar es salaam, yapo yanayofanywa na vijana wa bodaboda, hao pia ni miongoni mwa marafiki wa raisi? Vipi juu ya vijana waendesha bodaboda ambao hawafuati taratibu za barabarani na wakipata ajali wanakurupuka na kumshambulia mwenye gari ambaye hana hatia na wakati mwingine kumsabibishia kifo, au kuchoma vituo vya polisi kwa kuingilia maamuzi yao mabovu, je nao ni miongoni mwa marafiki wa raisi? Vipi kuhusu wale wasiosimama wakati taa nyekundu zikiwaka au traffic akiongoza magari ktk upande tofauti nao kutotii amri au taratibu husika nao ni miongoni mwa marafiki zako mheshimiwa?
- Kingine ambacho baadhi ya wagombea ambacho hawakukifanyia utafiti maana hawajawahi kuishi katika jamii ni kuwa kijana wa bodaboda au mama lishe unayeongea naye yeye si mmiliki wa hiyo bishara! yeye katumwa tu, yawezekana nyinyi nyinyi mnaopiga kampeni, sisi vifisadi wadogo au wajanja wachache ndio wanaowamiliki! wengi wanaopigwa jua, kukatwa miguu kwa ajali wakiingia town bila ya kujua sheria za usalama sio wamiliki, wanaambulia buku 2 tu usiku. Waheshimiwa tuulizeni kwanza kabla hamjatuzungumzia. No wonder baadhi yao wanakwepa midahalo.
- Mi nadhani waheshimiwa wagombea badala ya kuwashabikia mama ntilie, bodaboda, wamachinga, wahasibu, madaktari au walimu etc kuwa nao kundi moja na kuwakumbatia wema na waharifu, wagombea wasimame kidete na kuwahamasisha makundi mbalimbali ya kijamii kufanya shughuli zao kwa kufuata misingi, kanuni na taratibu za taaluma au shughuli hizo, kuzingatia usalama kwa wananchi wote na sio mkuu wa nchi kutaka kudharau taratibu zilizowekwa kwa manufaa yako binafsi na kuweka rehani maisha ya wananchi waliowengi.
Kwa taswira hii naogopa yawezekana siku akaingia kiongozi atakayeona huitaji wa kuwa na kundi la maharamia, je tutaipeleka wapi nchi yetu? ni kweli Tanzania hii inaweza kuendeshwa bila ya kufuata taratibu?
Najua wengi wetu walikuwa wakidhani amani tuliyonayo leo imekuja kwa bahati nasibu, hawaoni kuwa kuna haja ya viongozi kuandaa mikakati thabiti ya kuilinda na kudumisha amani yetu kwa kufuata sheria na taratibu tena sote tusimamie kwa nguvu zetu zote!
Naomba niige kibwagizo cha Ally Choki (ukiwaunaona elimu ni ghali basi jaribu ujinga) na wewe ukiona amani ni ghali basi chagua viongozi wa aina hizo nilizotaja hapo juu.