nanjilinji
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 1,206
- 566
inaonyesha na wewe wamo si habaUkimpenda mtu utamthamini na kumuheshimu pia
inaonyesha na wewe wamo si habaUkimpenda mtu utamthamini na kumuheshimu pia
Memba na weye kitambi vipi? Kulakula ni hatari kwa afya
Roho dhaifu hii
Ikemee
Memba na weye kitambi vipi? Kulakula ni hatari kwa afya
Sawa ila kitambi ni kula kula tu. Hakuna shaka ke hata me vitambi its a result of over feeding aisee. Wenzetu wanapunguza vitambi kwa kupunguza kufakamiaSio kila anyeposti ana kitambi kama wewe
Hapa kinachotokea ni roho mbaya uchoyo na kukosa adabu Chakula ni mavi tu Badilisha tabia yako
Ila unene mwingine si wa kula ni kuridhika jamani....Kuna mtu mnene lkn ukiona anachokula utashangaa kilivyo kidogo....NDIO MAANA ISSA MATONA AKAIMBA : MTU MWENYE TUMBO DOGO KWA KULA HAWEZEKANI...
Wasiokuwa na matumbo ndio walaji wakuu ila miili hairidhiki...
Mabonge watamu wewe, halaf wanaridhika haraka, hawana na makuu ninachowapendea ni wepesi wa kusamehe na kusahauSasa huyo rafiki yako mi nlidhani atafurahi mkewe akisema anaondoka ili ajibebee kipotabo kwa raha zake
Mabonge watamu wewe, halaf wanaridhika haraka, hawana na makuu ninachowapendea ni wepesi wa kusamehe na kusahau
Mi nashauri Jando na Unyago virudishwe kama Jk alivyorudisha Jeshi baada ya F6. Wanandoa wengi hawajakua na hawana uelewa wowote juu ya ndoa na hata heshima kwa jamii. Yani ni weupe kabisa kichwani!!!
Mtu mwenye akili timamu anawezaje kushushia heshima mkewe kiasi hicho? Tena mbele ya mgeni!
Halafu huyo mkewe akijapata rafiki wa kiume anayemkubali alivyo na kumsifia akachepuka mtarudi hapa kutuomba ushauri. Kila mtu hustahili kuthaminiwa na kuheshimiwa...na mwanandoa ndiye mstari wa mwisho kwenye hayo mambo. Sasa mtu ulalala naye na kumhudumia kisha humthamini, akichepuka kwenda kutafuta usichompa utamlaumu nani?
Lakini kuna wanawake wanapakia sana jamani khaaa? mtu unanunua chakula ndani cha mwezi, kinakaa wiki na nusu!! huyo ni mke au pipa? halafu anafutuka balaa na magonjwa ya moyo hayoo!!
kama ujamalizia hapo..... asingemtania mbele yako? badae labda ila na unakulaje mpaka uvimbe vimbe hovyo......ha ha ha ha yani nimetafakari jamani huyu mnyama anashape mbaya ningejiua loh....... jamaa hakutenda haki kabisa
View attachment 197418View attachment 197420View attachment 197421
Siyo kwenye ndoa tu mkuu,mi nilikuwa na mwanangu
tukaenda ofisi fulani,sasa wakati nawatambulisha wale wafanyakazi kuwa huyu ni mwanangu.
mmama mmoja akamwambia mwanangu kwamba mimi ndo mchepuko wa baba yako,huku akijua sijawahi kuongea naye chochote.
Kwa kweli nilijisikia vibaya.Hivyo ni muhimu kupima unataka kumtani mtu katika jambo gani na ni mazingira yapi.
Picha iliyopo kichwani mwangu siku zote juu yako Miss Chagga ni kuwa wewe ni kibonge flani hivi.
Yani mwenye minyama ya uzembe
Ama najidanganya?- Usiniambie kuwa wewe ni kimbaumbau.
Jana jioni nimemtembelea rafiki yangu mmoja. Huyu jamaa huwa haishi kulalama kuhusu tabia ya ulaji ya mkewe na kujiachia jambo linalofanya avimbiane kuliko kawaida. Sasa wakati tunapiga story, kulikuwa na ka-documentary fulani kwa Tv kanazungumzia maisha ya viboko (Wengi huwaita boko).
Basi jamaa akamuita mkewe kama ana jambo fulani muhimu vile; "We mama H njoo mara moja".
Wife kafika jamaa anamuonesha Tv eti "Si unawaona ndugu zako hao wanavyojiachia hapo." Sokomoko lililoanguka ilibidi niage, jamaa ananimbia hadi sasa ushwari haujarejea. Wife anadai jamaa akaoe hao vipotabo ye aondoke.
Jamani busara zizingatiwe yanapokuja masuala ya mizaha haya.