Kuna utani unaweza kuvunja ndoa

Kuna utani unaweza kuvunja ndoa

MNYAMAKAZI

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2014
Posts
2,118
Reaction score
2,198
Jana jioni nimemtembelea rafiki yangu mmoja. Huyu jamaa huwa haishi kulalama kuhusu tabia ya ulaji ya mkewe na kujiachia jambo linalofanya avimbiane kuliko kawaida. Sasa wakati tunapiga story, kulikuwa na ka-documentary fulani kwa Tv kanazungumzia maisha ya viboko (Wengi huwaita boko).

Basi jamaa akamuita mkewe kama ana jambo fulani muhimu vile; "We mama H njoo mara moja".

Wife kafika jamaa anamuonesha Tv eti "Si unawaona ndugu zako hao wanavyojiachia hapo." Sokomoko lililoanguka ilibidi niage, jamaa ananimbia hadi sasa ushwari haujarejea. Wife anadai jamaa akaoe hao vipotabo ye aondoke.

Jamani busara zizingatiwe yanapokuja masuala ya mizaha haya.
 
kama ujamalizia hapo..... asingemtania mbele yako? badae labda ila na unakulaje mpaka uvimbe vimbe hovyo......ha ha ha ha yani nimetafakari jamani huyu mnyama anashape mbaya ningejiua loh....... jamaa hakutenda haki kabisa
kiboko.png kiboko 3.jpg kiboko 4.jpg
 
Mi nashauri Jando na Unyago virudishwe kama Jk alivyorudisha Jeshi baada ya F6. Wanandoa wengi hawajakua na hawana uelewa wowote juu ya ndoa na hata heshima kwa jamii. Yani ni weupe kabisa kichwani!!!
Mtu mwenye akili timamu anawezaje kushushia heshima mkewe kiasi hicho? Tena mbele ya mgeni!
Halafu huyo mkewe akijapata rafiki wa kiume anayemkubali alivyo na kumsifia akachepuka mtarudi hapa kutuomba ushauri. Kila mtu hustahili kuthaminiwa na kuheshimiwa...na mwanandoa ndiye mstari wa mwisho kwenye hayo mambo. Sasa mtu ulalala naye na kumhudumia kisha humthamini, akichepuka kwenda kutafuta usichompa utamlaumu nani?

Wife anadai jamaa akaoe hao vipotabo ye aondoke. Jamani busara zizingatiwe yanapokuja masuala ya mizaha haya.
 
Mi nashauri Jando na Unyago virudishwe kama Jk alivyorudisha Jeshi baada ya F6. Wanandoa wengi hawajakua na hawana uelewa wowote juu ya ndoa na hata heshima kwa jamii. Yani ni weupe kabisa kichwani!!!
Mtu mwenye akili timamu anawezaje kushushia heshima mkewe kiasi hicho? Tena mbele ya mgeni!
Halafu huyo mkewe akijapata rafiki wa kiume anayemkubali alivyo na kumsifia akachepuka mtarudi hapa kutuomba ushauri. Kila mtu hustahili kuthaminiwa na kuheshimiwa...na mwanandoa ndiye mstari wa mwisho kwenye hayo mambo. Sasa mtu ulalala naye na kumhudumia kisha humthamini, akichepuka kwenda kutafuta usichompa utamlaumu nani?

Kwani jando na unyago vimefutwa?? mbona huku lindi na mtwara tunaendeleza
 
Jana jioni nimemtembelea rafiki yangu mmoja. Huyu jamaa huwa haishi kulalama kuhusu tabia ya ulaji ya mkewe na kujiachia jambo linalofanya avimbiane kuliko kawaida. Sasa wakati tunapiga story, kulikuwa na ka-documentary fulani kwa Tv kanazungumzia maisha ya viboko (Wengi huwaita boko). Basi jamaa akamuita mkewe kama ana jambo fulani muhimu vile; "We mama H njoo mara moja". Wife kafika jamaa anamuonesha Tv eti "Si unawaona ndugu zako hao wanavyojiachia hapo." Sokomoko lililoanguka ilibidi niage, jamaa ananimbia hadi sasa ushwari haujarejea. Wife anadai jamaa akaoe hao vipotabo ye aondoke. Jamani busara zizingatiwe yanapokuja masuala ya mizaha haya.

Lakini aisee hawa mabonge wanatandika menyu! Usije kaa naye karibu utastaajabu tu!
 
Lakini kuna wanawake wanapakia sana jamani khaaa? mtu unanunua chakula ndani cha mwezi, kinakaa wiki na nusu!! huyo ni mke au pipa? halafu anafutuka balaa na magonjwa ya moyo hayoo!!
 
Ha ha haaa kweli utani mwingine ni mbaya. Ndo amfananishe mkewe na kiboko?
 
Aisee sipendi utani wa kijinga, huyo hana hata heshima hata kama anakula sana ndio amfananishe na mnyama.
 
Hahhaahah jaman mbona mnatusemaa ndo tusileee?embu mtuachee#mabonge

Kwa kweli watuacheeee!!! Na siyo wote wenye kupenda kula wapo vipotabo na wanakula kuliko,wengine ni kina bonge nwepesi.
 
Hamna kitu mbaya kama kumtania mwanamke kuhusu maswala ya uzito na unene, mwanamke anataka hata mnene vp anakaribia kupasuka umwambie yupo kawaida tu
 
kiboko ha ha ha ha ha ha ha

aiseee.....

nimecheka hadi basi
 
yaani na me ningehakikisha namuaibisha balaa maneno gani hayo mbele ya watu alipaswa amwambie kwa upendo kuhusu kufanya diet na amsaidie afanye mazoezi. ingekuwa mie ningemwambia dia na we jitahidi basi ukaongeze hicho kibamia chako maana hakiniridhi kabisa aone uchungu wake
 
Siyo kwenye ndoa tu mkuu,mi nilikuwa na mwanangu
tukaenda ofisi fulani,sasa wakati nawatambulisha wale wafanyakazi kuwa huyu ni mwanangu.
mmama mmoja akamwambia mwanangu kwamba mimi ndo mchepuko wa baba yako,huku akijua sijawahi kuongea naye chochote.
Kwa kweli nilijisikia vibaya.Hivyo ni muhimu kupima unataka kumtani mtu katika jambo gani na ni mazingira yapi.
 
Nimekupenda kweli..
Vitu vingine vyahitaji busara

Mi nashauri Jando na Unyago virudishwe kama Jk alivyorudisha Jeshi baada ya F6. Wanandoa wengi hawajakua na hawana uelewa wowote juu ya ndoa na hata heshima kwa jamii. Yani ni weupe kabisa kichwani!!!
Mtu mwenye akili timamu anawezaje kushushia heshima mkewe kiasi hicho? Tena mbele ya mgeni!
Halafu huyo mkewe akijapata rafiki wa kiume anayemkubali alivyo na kumsifia akachepuka mtarudi hapa kutuomba ushauri. Kila mtu hustahili kuthaminiwa na kuheshimiwa...na mwanandoa ndiye mstari wa mwisho kwenye hayo mambo. Sasa mtu ulalala naye na kumhudumia kisha humthamini, akichepuka kwenda kutafuta usichompa utamlaumu nani?

Ila unene mwingine si wa kula ni kuridhika jamani....Kuna mtu mnene lkn ukiona anachokula utashangaa kilivyo kidogo....NDIO MAANA ISSA MATONA AKAIMBA : MTU MWENYE TUMBO DOGO KWA KULA HAWEZEKANI...
Wasiokuwa na matumbo ndio walaji wakuu ila miili hairidhiki...

Lakini kuna wanawake wanapakia sana jamani khaaa? mtu unanunua chakula ndani cha mwezi, kinakaa wiki na nusu!! huyo ni mke au pipa? halafu anafutuka balaa na magonjwa ya moyo hayoo!!
 
Lakini kuna wanawake wanapakia sana jamani khaaa? mtu unanunua chakula ndani cha mwezi, kinakaa wiki na nusu!! huyo ni mke au pipa? halafu anafutuka balaa na magonjwa ya moyo hayoo!!
Dah,mkuu hii siyo sawa kabisa,mambo ya chakula tena!
Vijana nawashauri kabla hamjaoa lazima kujipanga,coz ukiwa peke yako
hata kilo 5 za mchele unaweza kaa nazo hata mwezi mzima,kwa sababu ya uvivu wa kupika
sasa umeoa, mkeo anakupikia kila siku,mchele ukipungua unasema anakula sana,
Kweli shukrani ya punda ni mateke.
 
Hahahaaaaaaaa, mbavu zangu jamani, eeh hata kama ni kutaniana kumevuka mipaka yn hadi wageni wakiwepo mtu unaona sawa tu, tehtehteeeeeeeh. Yn iii kila nikikumbuka ntakua namwagika mbavu.
 
Jana jioni nimemtembelea rafiki yangu mmoja. Huyu jamaa huwa haishi kulalama kuhusu tabia ya ulaji ya mkewe na kujiachia jambo linalofanya avimbiane kuliko kawaida. Sasa wakati tunapiga story, kulikuwa na ka-documentary fulani kwa Tv kanazungumzia maisha ya viboko (Wengi huwaita boko). Basi jamaa akamuita mkewe kama ana jambo fulani muhimu vile; "We mama H njoo mara moja". Wife kafika jamaa anamuonesha Tv eti "Si unawaona ndugu zako hao wanavyojiachia hapo." Sokomoko lililoanguka ilibidi niage, jamaa ananimbia hadi sasa ushwari haujarejea. Wife anadai jamaa akaoe hao vipotabo ye aondoke. Jamani busara zizingatiwe yanapokuja masuala ya mizaha haya.

Pamoja na kuwa na siku yenye changamoto nyingi kwa leo nmejikuta kuja huku kunaamshafuraha isiyo kifani, nadhani ofisini wameniona km nimerukwa kwa jinsi nilivyocheka. Km nilikuwepo vile
 
Back
Top Bottom