Kuna usalama hapa? Maoni yako ni muhimu

Kuna usalama hapa? Maoni yako ni muhimu

umemaliza mjadala closed.
Bado Boss...

Tusubirie subirie tuzidi kupata elimu...teknolojia imeingia kwa kasi sasa cha muhimu ni kupambana nayo usiku + mchana ili tuelimike.

Kwa sabbu sisi sio kisiwa,lazima tukubaliane na hali ilivyo..ukisasa umekuwa + kuwepo kwa mafundisho mengi ya dini yakielezea mahusiano.Wengine wanapinda pinda hawaeleweki ndio maana nimeleta bandiko hapa tujifunze
 
Ni lini hasi na Chanya zikigusana isitokee shoti???.

Mambo ya Boy na Girl friends ni utamaduni wa kimagharibi, utamaduni huo hautokani na misingi ya ukristo.

Yesu anasema; "Si imeandikwa usizini, amin nawaambia mtu akimtazama mwanamke na akamtamani atakuwa amezini---"

Sasa nikuulize inawezekanaje Boy na Girl friends wakae tu kama marafiki bila kutamaniana??!

Katika Qur'an imeandikwa; "wala msikaribie zinaa hakika hicho ni kitendo kichafu"

Hapo Qur'an ndiyo imefunga kazi kwa kusema Msikaribie zinaa sio msizini bali msikaribie yaani tuepuke njia zote zinazoweza kutupeleka katika zinaa.


Hakuna urafiki kati ya msichana na mvulani pakawepo na "usalama".
 
Dini ipi hiyo inashauri hayo kua vijana wawe na rafiki wa kike na rafiki wa kiume? Braza stadi za maisha hizo umesomea wapi ?
Kuna Radio moja huku nilipo nilikuwa naisikiliza nikayasikia hayo maneno mpaka nikashtuka..how?..hata kipindi hicho nikiwa masomoni kuna mchungaji mmoja alikuwa anatoa ushauri + nasaha akadokezea hili jambo nikashangaa sana inakuwaje?

Ok ntakuletea tena picha hapa/clip ikielezea hayo yote.
 
Ni lini hasi na Chanya zikigusana isitokee shoti??
Shukrani sana Mkuu,umeelezea vizuri.

Kuna wengine huwa wanadai ni mume/me mtarajiwa huku wakiongozana...hawa tuwaweke kundi lipi?..au cha muhimu ni USALAMA?
 
Shukrani sana Mkuu,umeelezea vizuri.

Kuna wengine huwa wanadai ni mume/me mtarajiwa huku wakiongozana...hawa tuwaweke kundi lipi?..au cha muhimu ni USALAMA?
Kwa sheria ya kiislamu hiyo hairuhusiwi nadhani hata kwa mafundisho ya kikristo pia hairuhusiwi kama wapo wajuzi watufahamishe.

Msichana na mvulana mzizoeana kwa karibu sana hata ladha ya ndoa hupungua sana na mara nyingi mara baada ya kufunga ndoa ndoa za aina hiyo huwa hazidumu sana.
 
Back
Top Bottom