Kuna umuhimu mkubwa sana wa kila raia kujua haki zake kisheria!!

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
Jana Lissu na wenzake baada ya kufikishwa kituo cha Polisi Karatu mambo yalikua hivi;

LISSU: Mheshimiwa OCD mmetukamata kwa kosa gani?

OCD: Uchochezi.

LISSU: Lina dhamana au halina dhamana?

OCD: Unajua tatizo lenu Chadema ni kujifanya mnajua sana.

LISSU: Sio kujifanya. Soma sheria ya uchochezi namba 18 sura 455, kiifungu kidogo cha 2. Sheria inasemaje kuhusu kosa la uchochezi? Lina dhamana au halina dhamana?

OCD: Lina dhamana. Lakini leo ni jumapili, itabidi mtoke kesho.

LISSU: Fungua Police General Orders (PGO) ukurasa wa 16. Je inazuia mtu kupewa dhamana kwa sababu ni jumapili?

OCD: Hapana.

LISSU: Sasa hiyo ya kusema tutadhaminiwa kesho umeitoa wapi?

OCD: Unajua Mheshimiwa....

LISSU: Sikiliza bwana mkubwa. Hii PGO ndio muongozo wenu wa kazi kama ilivyo Biblia kwa Wachungaji/Mapadre na Quran tukufu kwa Masheikh. Mnatakiwa muijue vizuri.

OCD: Basi tafuta wadhamini wawili waje kukudhamini utoke.

LISSU: Nitajidhamini mwenyewe.

OCD: Haiwezekani.

LISSU: Fungua PGO ukurasa wa 7 kifungu cha 13 usome kuhusu makosa ambayo mtu anaweza kujidhamini mwenyewe. Na hili lipo. Sio?

OCD: (huku akicheka) sawa bwana, nendeni mrudi kesho saa 4 asubuhi.

Hivyo ndivyo Lissu na viongozi wenzie walivyoachiwa huru jana. Leo wameenda kituoni kuripoti kama OCD alivyoelekeza. Kujua sheria ni jambo muhimu sana. Watu wengi huonewa na kupoteza haki zao kwa kutokujua sheria
 
Huyo ni lissu sisi kina hamisi john na mwanaisha, seleman nk jichanganye utatandikwa virungu nk
 
Hakuna serikali ya africa itaacha hilo litokee na unaweza kujua sheria but at the end ukalala ndani vile vile.

Hyo sheria ina apply ukiwa mtu fulani au unajuana na fulani sisi wakina jamba nane ukimjibu hivyo na makofi juu utachezea huku ukiambiwa unanifundisha kazi
 
Inasikitisha sana
 
nacheka kama mazuri ila umeongea facts tupu mkuu

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Ahahahaha kujua sheria na haki zako ni moja, na kupata hizo hali ni suala tofauti kabisa.
 
Back
Top Bottom