Kuna umuhimu jaman,i wa ...........................

Ngo

JF-Expert Member
May 25, 2010
284
51
Wana JF

Ni kitu cha kawaida kwa mzazi kumkumbushia mtoto/kijana wake kuhusu suala la mapenzi na mihemuko inayowapata vijana katika umri wa kubarehe au niseme katika level ya sekondari na kurudi chini. Hata vyuoni pia wazazi wanakumbushia vijana kuwa makini katika ulimwengu wa sasa uliojaa vishawishi vya kila namna na athari ya magonjwa yaliyopo. Kwa upande mwingine kwa watu wengi walioko kwenye ndoa suala la kukumbushana hili jambo la kila partner kuwa makini linachukuliwa kuwa ni jambo linalojulikana tunakuwa na assumption kuwa wenzi wetu wako makini hawahitaji kukumbushiwa. Mwisho wake ndo tunaona watu walioowa au kuolewa bado wanazidi kutembea nje ya ndoa zao kama vile hawako katika ndoa. Mifano mingi kuhusu hili inaonekana mitaani na hata huko makazini.

Kwa upande wangu naonelea, na huwa tunakumbusha na mwenzi wangu kuwa makini kwa kuchukua taadhari zote zinazowezekana katika kulinda, kuimalisha na kuboresha uhusiano wetu wa mapenzi. Na hili kwangu mimi linafanya kazi maana huwa tunaongea kinagaubaga athari ya mmoja wetu kuwa na mausiano mengine pembeni na faida ya kuwa waaminifu. Imefika maali wengine wanaamua kwenda kukumbushia viapo kwa wachungaji.Wana JF watu waendelee ku-assume ''ukiwa kwenye mausiano unajua athari ya kutoka nje ya ndoa bila kukumbushana?' Hasa kwa wanandoa.
 
wengi wetu hatuongelei kabisa masuala ya mapenzi kwa ujumla wake kwa uwazi,binafsi sikumbuki baba kunitaadharisha na vishawishi ninavyoweza kukutana navyo katika safari yangu ya kuyaendea maisha,hatua gani za kuchukua na jinsi gani ya kujikinga na vishawishi hivi achilia mbali magonjwa yaliyotapakaa kila eneo.Naamini alikuwa anahisi ninajua kila kitu.Mama alijaribu hasa kuhusu ukimwi ingawa kwa sasa naona anakuwa too protective.Pia sikumbuki kukumbushana na mwenza wangu kuhusu suala hili,kila mmoja wetu akiamini mwenzake anajua umuhimu wa kutokutoka nje ya ndoa,nadhani kuna haja ya kukumbushana.we should never leave anything to chance.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom