Kuna Umuhimu gani wa ziara ya Obama hapa Tanganyika?

mbinguni

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
2,746
1,052
Ziara nyingi za hawa viongozi wa nchi za magharibi zinafanyika kwa malengo fulani.Malengo yao ni kupata rasilimali mbadala kwa ajili ya kuvilisha viwanda vyao ili kuzalisha kwa wingi na baadae kutugeuza kuwa masoko ya bidhaa zao.

Ziara hizi zinashadadiwa na viongozi wetu bila kujua madhara yake kwa wananchi.Matokeo yake ni watawala wetu kusaini mikataba feki mingi ya kutoa rasilimali zetu kwa bei za hovyo huku wao wakifunguliwa akaunti huko nje.

Itakuwa busara sana wananchi na hasa watanganyika tukashikamana bega kwa bega katika harakati hizi za kumng'oa mkoloni huyu mweusi ili tujikomboe rasmi na tuweze kuuaga umaskini kwani tuna rasilimali nyingi mno ambazo tukizitumia vizuri, tutatajirika kuliko taifa lolote katika sayari hii ya dunia.
 
Back
Top Bottom