Kuna umuhimu gani wa kuwa mwema?? (What is the essence of being a nice guy/person?)

GuyFromArusha

Member
May 10, 2016
71
82
Habari za Jumapili!!

Nimekaa hapa nikawa nawaza hivi ukiachilia mbali Vitabu vya dini vinavyotuasa kua watu wema na kuwatendea wenzetu vile ambavyo sisi tungependa kutendewa yote hii kwa ahadi ya kupata makazi ya milele mbinguni, hivi kuna umihimu wowote wa kuwa mtu mwema?

Nauliza hivi kwa sababu kuna watu wengi sana waovu, wagomvi, antisocial, arrogant lakini wanafanikiwa tu kimaisha na from the looks of it, they seem to be living an okay if not a great life.

..Je ni muhimu kusaidia mtu usiemfahamu kabisa?

..Ni muhimu kuonesha upendo kwa ndugu zako mara kwa mara (au ni kupoteza muda)?

..Ni muhimu kusikiliza na kushuhulikia matatizo ya watu unaowafahamu (au kupotezea na kuendelea tu na shuhuli zako)

.. Ni muhimu kutojihusisha na uhalifu ama wizi pale nafasi inapojitokeza? (Au labda nikutochangamkia fursa? )

Nakaribisha mawazo/ your reflections on the matter....
 
Back
Top Bottom