Kutoa dukuduku ni moja ya tiba kubwa sana,,mfano umeona kumbe sio wewe peke yako unayepitia au uliyepitia machungu,,kuna mwamba hapo ametoa ushuhuda jinsi alivyopitia machungu zaidi yako,,hiyo inasaidia kujua kuwa kuna wenzako kama wewe pia
Pili hisia za machungu au msongo hauondolewi na pombe au bangi unachofanya ni kuahirisha tatizo lkn stimu zikiisha tatizo liko pale pale
Wanashauri wataalamu hisia za machungu zikikujia husizikwepe kwa maana kama utahisi kulia basi lia na kama kuhuzunika basi huzunika,kwa kufanya hivyo zinapunguza makali na kuchukuliwa na subconscious mind yako kwamba hizo hisia sio tishio tena kwako hivyo zinakuwa familiar kwako na baada ya mda fulani kupita utakuwa okay
Kuhusu kipenz chako uliyempoteza kubali kwamba ni kazi ya mungu na mda wake ulifika,usijiweke katika lawama labda kama hasingeshika mimba huenda angekuwa hai,,hiyo ndio ilikuwa sababu ya kuondoka kwake
Kwahiyo maisha ndiyo yalivyo chief,,,lakini kama walivyosema wadau kama unahisi msongo unakuwa mkubwa waone wataalamu wakusaidie zaidi