Lundavi
JF-Expert Member
- Aug 11, 2016
- 327
- 323
Habari wanajukwaa: Kama kichwa kinavyoeleza, nimeingiwa na wasiwasi huo baada ya tatizo lililoikumba ndoa yangu. Tatizo hilo lilianza baada ya kuoa binti mwenye kundi la damu o- negative na Mimi nikiwa na o- positive. Kibaya zaidi hatukuwa tunalifahamu hilo kabla na tukalifahamu baada ya mimba mbili kuharibika. Baada ya kufuatilia katika maandiko mbali mbali ya kitabibu nikagundua kuwa tatizo limekuwa kubwa kwasababu mke wangu tayari mwili wake umesha "be sensitized " kwa mimba yoyote itakayotungwa na mtoto akawa na group o-negative LA damu. Na kwa mujibu wa maandiko hayo niliyoyasoma ni kwamba hata ile "Ant D injection " haitasaidia. Naomba kwa mwenye uelewa wa hili jambo anisaidie jamani. Muda mwingine nafikiria kuachana na huyu mke wangu lakini sidhani kama yupo anae mzidi kwa maadili aliyonayo huyu mke wangu. Karibuni jamani.