GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Za chini ya Kapeti kutoka katika Taasisi moja ni kwamba kumbe ' Mukulu ' mwenyewe kwanza alitaka mishahara yao ipunguzwe kwakuwa ni mikubwa halafu hata tija yao si kubwa kivile ila watangulizi wake wakamshauri kuwa asifanye hivyo kwani ingeweza kumletea shida kidogo hata yeye kwa ' ustawi ' wake kama ambavyo ilishawahi kutaka kumtokea mtangulizi wake namba mbili ( katikati ya kwa Mwalimu na kwa Warioba ) na akakubali kwa yeye pia kuwapa sharti ( hiyo taasisi ) kuwa kuanzia sasa hakuna ' Watumishi ' wake kupandishwa Vyeo na kwamba ameagiza hata mishahara yao ya sasa ibaki kuwa hii hii kwa muda wa miaka mitano ( 5 ) ijayo ndipo atawafikiria.
Baada ya kulisikia hili binafsi nikafanya ' kajiuchunguzi ' kangu kadogo tu na kuweza kuona dalili za ' kutukuka ' kabisa ya hizo taarifa nilizopewa za chini ya kapeti kwani ni ukweli sasa kuwa hao Watu sasa hivi......
Akhsante Mukulu na hii ndiyo Tanzania ya usawa ambayo siku zote sisi tulikuwa tunaitaka. Heko!

- Hawatongozi tena hovyo.
- Hawalewi hovyo.
- Hawapigi wenzao hovyo kwa jeuri yao ya pesa.
- Nyuma walikuwa wakihonga Mipesa ila sasa wanahonga Vijihela tu vya ngama.
- Wana adabu zote kwa wanajamii wanaowazunguka.
- Wanatulia majumbani mwao sana na wanawaheshimu mno Wake zao kuliko zamani.
- Wamekuwa ' wabahili ' sana na wamegeuka kuwa wapangaji ' bajeti ' wazuri mno.
Akhsante Mukulu na hii ndiyo Tanzania ya usawa ambayo siku zote sisi tulikuwa tunaitaka. Heko!