Kuna siri gani kwenye chumvi?

Kuna siri gani kwenye chumvi?

42774277

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2018
Posts
6,835
Reaction score
8,874
Mods naomba mtauweka uzi huu kwenye jukwaa sahihi kama nimekosea.

2 Wafalme 2:19-22

Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza. ndani yake.

Wakamletea. Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, BWANA asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza.

Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena.

Leo katika pitapita zangu nikakutana na video moja tiktok kuna mdada anaongea habari za chumvi, story za kuogea chumvi na kadhalika. Na kuna watu wanashuhudia kabisa zimework out kwao.

Pia nikakumbuka zile story za kama mtu mtu ana mikosi wanamshauri akaoge maji ya baharini atoe mikosi. Huenda kuna ukweli. Mimi sijajua.

Nikalazimika kutafuta kwenye biblia story za chumvi na ndio nikakutana na hiyo ya 2 Wafalme 2:19-22. Sijajua kwenye vitabu vya dini zingine kama imezungumzwa wenzetu mtatusaidia.

Kwenye bible inaonesha kumbe chumvi ilikuwa inatumika toka miaka hiyo kuponya vitu as kama ilivyo kwenye hiyo story ya wafalme.

Kuna siri gani kwenye chumvi?

Kama una nondo za kuongezea unaweza kutiririka.

Jumapili njema.
 
Chumvi ,maji na asali ni vitu ambavyo visipowekewa addiction yeyote haviharibiki

Chumvi Ina kausha
Maji yanaweka unyevu
Asali inatunza kitu katika muonekano wake

Trust Me duniani hamna dawa nje ya hizo vitu plus Maziwa ni kubalance ratio kutokana na mahitaji ya mwili wako tu
 
Mods naomba mtauweka uzi huu kwenye jukwaa sahihi kama nimekosea.

2 Wafalme 2:19-22

Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza. ndani yake.

Wakamletea. Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, BWANA asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza.

Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena.

Leo katika pitapita zangu nikakutana na video moja tiktok kuna mdada anaongea habari za chumvi, story za kuogea chumvi na kadhalika. Na kuna watu wanashuhudia kabisa zimework out kwao.

Pia nikakumbuka zile story za kama mtu mtu ana mikosi wanamshauri akaoge maji ya baharini atoe mikosi. Huenda kuna ukweli. Mimi sijajua.

Nikalazimika kutafuta kwenye biblia story za chumvi na ndio nikakutana na hiyo ya 2 Wafalme 2:19-22. Sijajua kwenye vitabu vya dini zingine kama imezungumzwa wenzetu mtatusaidia.

Kwenye bible inaonesha kumbe chumvi ilikuwa inatumika toka miaka hiyo kuponya vitu as kama ilivyo kwenye hiyo story ya wafalme.

Kuna siri gani kwenye chumvi?

Kama una nondo za kuongezea unaweza kutiririka.

Jumapili njema.
Share hiyo link ya video
 
Chumvi na maji ni natural elements zilizobeba siri nyingi na kubwa kwa viumbe hai(maji ndio uwanja wa chumvi kufanya kazi).
Chumvi na maji vina nguvu za kuondoa uchafu, kuponya, kukuza, kuhifadhi vitu mbalimbali n.k.
Baadhi ya Imani za dini mfano Katoliki hutumia sana maji na Chumvi kwenye Ibada, kabla ya Corona ilikuwa lazima kwa waumini kujichovya kwa maji yaliyobarikiwa kwa Chumvi kabla na baada ya Ibada(huitwa MAJI YA BARAKA). Padre akienda kusoma misa Nyumbani kwa muumini lazima anyunyizie MAJI ya BARAKA kila mahali.
Hata vyakula vyetu vingi vimechanganywa na Chumvi.
Aina moja wapo ya Chumvi (NaCl) ni maarufu kwa sababu ndiyo tunayoitumia jikoni na mezani lakini watalam viwandani wanatengeneza aina mbalimbali za chumvi kwaajili ya mimea na wanyama.
Weka kwenye maji ya kunywa, kuogea, ukiwa na mashaka na bundi nayelia karibu yako iweke kwenye mkaa unaowaka. Wewe tumia tu Chumvi, yenyewe itafanya kazi regardless unaelewa na kuamini au lah!
 
mashanajr nakuomba hapa kunaswala linahitaji ufafanuzi maana hata waganga wakienyeji,wachungaji wanaoponya wanatumia sana chumvi sijaelewa ila katika bible kunamaali Ruth alikatazwa asigeuke alipogeuka akawa jiwe la chumvi iko sababu hapa.
Hivi mke wa Lutu alipogeuka nguzo ya chumvi ni nani aliyegeuka nyuma kuthibitisha kuwa aligeuka nguzo ya chumvi
 
chumvi ni madini meupe yanayotumiwa kwa kutiwa ndani ya chakula ili kukipa radha .kazi ya chumvi katika mwili kuimarisha mifupa na zipo nyingi.sasa katika ulimwengu wa roho.kuna siri kubwa ukisoma kwenye biblia umeona na kifungu umetaja waf2;20 utaona chumvi inavyo fanya kazi.hili jambo linaendana na imani.ukisoma wabre11;1.inasema hivi iman ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiayo ni bayana ya mambo yasioonekana.neno zito hapo ni yasio onekana.yaani kuna mambo yanaonekana lakini yapo mengi yasionekana na yanakisi katika ulimwengu wa mwili.narudi kwenye chumvi.ukiambatanisha na imani chumvi katika ulimwengu wa roho inaharibu,inaozesha,inavunja,inateketeza,.Lakini inaweza kuwa kinyume yake kulinga na uitaji na maombi unayo yaomba.
 
Back
Top Bottom