Kuna siri gani hapa

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,369
Kabla ya kuuliza swali langu nitataka watu wasome kwanza kitabu hiki

Mathayo 4

8 Kwa mara nyingine shetani akamchukua Yesu mpaka kwenye kilele cha mlima mrefu akamwonyesha milki zote za dunia na fahari zake, 9 kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote kama ukipiga magoti na kuniabudu.”

Swali langu ni hili

Kama shetani ndo anatoa utajiri kwanini sasa tunamuomba Mungu atupe utajiri na wakati utajiri upo mikononi mwa shetani?

Na kwanini Mungu alimpa shetani hayo yote? Uku akijua viumbe vyake vinataka maisha mazuri
Alitegemea nini

Hapa ndipo nashindwa kuelewa haya mambo ya dini
 
Utajili alopewa bin ADAM, wife akamega tunda kwa tamaanna akampa msela naye akaona isiwe tabu akapiga bite moja matata akasema ewala.
Bwana Godi akamchomoa EDEN akamsweka huko akateseke so dingi SHEIKH-Twani akawa ashabeba utajili.

Bwana YESU alipokata ubinadamu (alipokufa) pale on the Cross katundikwa kama kitoweo msalabani ndo akaenda moja kwa moja kwa bwashemeji SHEIKH-TWAN akanyang'anya funguo za mamlaka ya kuimiliki DUNIA na vyote vilivyomo skarejesha kwa BIN-ADAMU. So utajili uko kwa wanadamu wenyewe ni juhudi, maalifa na maisha tu ndio vinakupa utajili. Kile kinachofanyika kwa sheiktwan ni kiini macho ila hakunaga utajili. Ndio maana ukotoka kwake lazima vyote vipukutike na wewe ufe ila ukitafuta mwenyewe unaishi mpk unakufa watoto wanaendelea utajili.
Naamini umeelewa sasa kaza kichwa na uvivu wako ukaloge
 
Dunia ni.mali ya shetani. Alitupwa huku kama adhabu so shetani akaistudy vzr na kueewa. Cha ajabu Mungu naye akamleta dunia binadam kama adhabu ya kutomtii kule eden. Binadam amekuja duniani wakati tayari shetani na malaika waasi wengine ni watawala huku. Kwaio ya hapa duniani yote ni ya sheitwan. Kushindana na shetani ni sawa na swala kushindana na mamba akiwa kwenye maji.
 
Shetani akikupa Mali zinakuja na majuto, Pia ujue kwamba shetani aliumbwa na Mungu (aliitwa LUSIFA), unaweza kuona Nani senior hapo 😁ni sawa na mtoto wa mfalme aende kuongea na kiongozi aliyeasi halafu amwambie nitakupa hii sehemu ukininyenyekea 😁😁Hii ni joke kwa sababu anajua vyote vinamilikiwa na Mungu.

Utajiri usio na majuto unatoka kwa Mungu. Kumb 8:18 Nawe utamkumbuka BWANA Mungu wako maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri
 
1 YOHANA 5:19;"TUNAJUA TUNATOKANA NA MUNGU,LAKINI ULIMWENGU MZIMA UNAKAA KATIKA NGUVU ZA YULE MWOVU."
Ina maana ya kuwa ulimwengu unatawaliwa na ibilisi. Na kwa kwel hali zinaonyesha hvyo..
 
Shetani ni mmiliki wa dunia KWA muda. Dunia ni makazi ya mwanadamu KWA muda, makazi ya milele ya mwanadamu ni paradiso na jehanamu.
Shetani na mwanadamu wapo duniani KWA muda.
Mungu anaishi milele na si Dunia tu ndio yenye viumbe alivyoumba MUNGU bali kuna sayari zingine zenye uhai pia. Dunia ni kisehemu tu.
 
Kabla ya kuuliza swali langu nitataka watu wasome kwanza kitabu hiki

Mathayo 4

8 Kwa mara nyingine shetani akamchukua Yesu mpaka kwenye kilele cha mlima mrefu akamwonyesha milki zote za dunia na fahari zake, 9 kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote kama ukipiga magoti na kuniabudu.”

Swali langu ni hili

Kama shetani ndo anatoa utajiri kwanini sasa tunamuomba Mungu atupe utajiri na wakati utajiri upo mikononi mwa shetani?

Na kwanini Mungu alimpa shetani hayo yote? Uku akijua viumbe vyake vinataka maisha mazuri
Alitegemea nini

Hapa ndipo nashindwa kuelewa haya mambo ya dini
Muombe kwanza Mungu Roho Mtakatifu ili akuangazie uweze kuelewa Neno lake.Biblia sio km hadithi za akina Shigongo.
 
Mwanadamu alikuwa Eden . Shetani alikuwa mbinguni wote baada ya kutenda dhambi wakatupwa duniani makao ya mda Ili wafanye toba.
 
Kama shetani ndo anatoa utajiri kwanini sasa tunamuomba Mungu atupe utajiri na wakati utajiri upo mikononi mwa shetani?

Na kwanini Mungu alimpa shetani hayo yote? Uku akijua viumbe vyake vinataka maisha mazuri
Alitegemea nini
Chukua mfano rahisi wa maisha ya mtanzania anavyogombaniwa na ilani za vyama vya siasa

Wengina wanalamba asali na wengine wanasindikiza asali inayolambwa upande mwingine wanapinga ulamba asali kwa kuwaambia wafuasi fanyeni hivi na vile wao wakiwa masafa
 
Na tumuumbe mtu kwa mfano wetu.
Mwanadamu ni mkubwa kuliko hata huyo shetan na anauwezo wa kuumba chochote na kikawe. Anauwezo wa kuomba chochote toka kwa Baba na akapata.
Mungu ameumba vyote uvionavyo. Hili shetan kusema atakupa ni kiini macho maana kiuhalisia hakuma mali itokayo kwa mwovu ibilisi iliyowah kudumu.

Weng wamepata mali za kishetani ila hakuna iliyowah kumwacha salama. Kwahiyo vyote atoavyo shetani ni viini macho tu.

Mkiwa na iman mnaweza kuuambia mlima huu ng'ooka nao uka ng'ooka.

Mkuu biblia nadhan n ngumu kuielewe sana kama hutaisoma zaid ya mara moja na kutuliza akil
 
Mungu ni roho hivyo anatawa ulimwengu wa roho. Sio kwamba hana mamlaka kwenye ulimwengu wa mwili bali alichagua mwanadamu atawale ulimwengu wa mwili kwa niaba yake. Bustanini Eden alikua anamtembelea Adam kila siku kuongea nae kuhusu mambo mbalimbali. Shetani pia ni roho na baada ya kutupwa ulimwenguni alibaki kwenye roho akiwa hamiliki chochote ila akapewa muda kabla ya hukumu kwa kosa alilolifanya huko mbinguni. Ili Mungu atawale dunia anamhitaji binadamu na ili shetani atawale dunia anamhitaji binadamu. Shetani kwa kujua haya akamrubuni mwanadamu afanye kosa ili auchukue umiliki wa dunia kutoka mikononi mwa mwanadamu. Baada ya kuitii sauti ya shetani Adam akawa amempa umiliki wote aliopewa na Mungu. Ikabaki ili upate chochote kutoka kwa Mungu lazima utoe sadaka na maombi kwake na kwa shetani vivyo hivyo. Hakupi bure, anatoa kwa gharama. Gharama ya nafsi yako. Anahitaji vessel ya kuingia duniani na kufanya mambo yake na Mungu vivyo hivyo anahitaji vessel ya kuingia ili kueneza ufalme wake. Inategemeana upo upande wa nani. Mwishoni kuna malipo kwa anili ya vyote. Ukimchagua Mungu kuna malipo na shetani pia kuna malipo. Yesu alieza kishinda tamaa akatuonesha namna ya kushinda kupitia damu yake na matendo yake. Kikubwa ni imani yetu kwake. Usipoamini utahukumuwa. Ukiamini ujapokufa utakuwa hai milele na milele.
 
Back
Top Bottom