Kuna 'plundering' inaendelea kwenye shule na watawala wapo kimya

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,472
8,692
Janauary inakaribia na watoto waanze shule wale wanaoanza Form 1 na wale wanaoanza Standard one.

Ila kuna uharamia wa wazi wazi kabisa unafanyika na wakuu wako kimya kabisa.

1. Watoto kuambiwa wapeleke zana kama majembe, mafyekeo, panga. Kila mwaka hivi vitu hupelekwa na Form 1 na shule ukiangalia mazingira ya shule haina hata sehemu ya kulima bustani. Haina shamba wala nini.

Je hivi vitu huenda wapi? Kuna ukaguzi unaofanyika?

2. Watoto kuambiwa waende na sabuni za unga na hutajiwa brand kabisa inayotakiwa.

3. Watoto kuambiwa waende na rim paper hii unaweza dhania shule ina mitambo ya kuprint. Hebu fikiria shule ina wanafunzi 500 then rim paper 500 zinafanya nini? Kuna mitambo ya kuchapa magazeti hapo shuleni?

4. Watoto kulipa ada na hapo hapo wanalipishwa michango mingine.
- Mchango wa Majengo
- Matibabu
- Michezio
- Graduation
- Chakula na kadhalika
- Pesa ya uniform inakuwa ni juu mno utadhani kitambaa kinaagizwa Italy.
- Michango ya vitu kama Tshirt, tracksuits, sweta na kadhalika inakuwa iko inflated na mwisho wa siku wanapewa vitu visivyo kuwa na quality.

Je kazi ya ada kama ada ni ipi? Je kwa nini watoto wanalipishwa ada na hapo hapo wanalipishwa michango mingine? Nini kazi ya ada kwenye mashule?

Kuna wizi unafanyika sana na ni siku nyingi sana na watawala wako kimya kabisa.
 
Inaonekana mwanao unataka aende private ndio maana unasema unalipa ada!!

Hatujajua iyo adda ni shingapi, maana shule za serikali zote ni bure, kinachofanywa nikupokea mtoto tuuu!!!

Lakini Yote hii ni sababu ya kuzaa zaaa bila utaratibu, ila kama ungekuwa umezaa kwa kujiandaa na unataka mwanao apate elimu bora na una jua unawajibu kwake unge peleka hayo mahitaji na ukafatilia kila mara kama kweli vinamsaidia mwanao,

lakini kwakuwa mnazaaa zaaa tu na hamjui mtawasaidiaje hawa watoto kila siku ni kulalamika!!

Ulizaa mwenyewe pambana kama baba au mama mwanao apate elimu!!


Humu kuna watu watoto wao wanasoma shule za adda ya 20 milion wewe fyekeo tu lina kuuuuma
 
Write your reply...acha umbea basi uache unafki kabisa hivo vitu ni vya kueka mazingira safi au hadi hilo msaidiwe daah basi peleka private mishahara yenyewe inatusumbua na wewe mzazi utusumbue
 
Back
Top Bottom