Kuna ongezeko kubwa la watu mahakamani

Kuna ongezeko kubwa la watu mahakamani

mugere

Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
18
Reaction score
2
Ninaona sasa kuna ongezeko la kutisha la watu mahakamani.Mahakama zinafurika.Nimejiuliza mambo mengi kwa kuwa nilitegemea kutokana na kasi ya sasa hivi viashiria vya wateja wa mahakama kushuka angalau.Mahakama za mwanzo zinakuwa full muda wote,mpaka wakati mwingine mpaka saa 11 za jioni,baada ya muda wa kazi wa serikali.Vivo hivyo mahakama za Wilaya. Ninahisi sasa kuna haja ya kutafuta ufumbuzi wa kuchuja sasa mashauri yanayopaswa kuishia polisi,kwenye vitongoji,wenyeviti wa vijiji na hata mabaraza ya ardhi ya kata na vijiji. Kuna haja ya Check and balance ya muhimili wa sheria na pia sheria-jamii.Tija kwa kumaanisha nguvu kazi itapungua kwa maana ya uzalishaji.Watu wataishia kudai haki ndogo ambazo inahitaji usuruhishi tu.Magereza zitajaa na kuiongezea serikali mzigo maana hakuna njia ila vifungo gerezani au vifungo vya nje.
Utekelezaji wa sheria na sheria jamii viwe at equlibrium na mambo yataenda.
Hii labda ijengewe mkakati mpya kama emergence! Maana wenyeviti wa vijiji na vitongoji hawana kazi sasa! Watendaji wa vijiji na kata sasa ni makamisaa! Mambo hayaendi sasa.Swala sio kumaliza migogoro kwa kufunga ila hitajika partcipatory approach ya crime na dispute control. La sivyo ni kazi!
 
Sasa kama wenyeviti wa serikali za mitaa wamenyang'anywa mihuri ya serikali, vyanzo vya mapato ktk halmashauri sasa hivi vinasimamiwa na serikali kuu unategemea nini?
Lazima halmashauri na zenyewe zijitue mizigo yao na kuielekezea hukohuko serikali kuu.
 
Hao Wenye viti vya serikal kazi yao kwa sasa ni kutuandikia barua ya utambulisho wa mtaa basi, ngoja tumalizane na la viwanda kwanza tutarudi kuwaongezea majukumu mengine
 
Sasa kama wenyeviti wa serikali za mitaa wamenyang'anywa mihuri ya serikali, vyanzo vya mapato ktk halmashauri sasa hivi vinasimamiwa na serikali kuu unategemea nini?
Lazima halmashauri na zenyewe zijitue mizigo yao na kuielekezea hukohuko serikali kuu.
Tuko bize na viwanda kwanza watuache wenyevit vya serikali
 
ni kwasababu tu mgeni mahakamani, ila kwetu sisi ambao tunaspend muda mwingi mahakamani kuliko hata nyumbani, tunaona kawaida tu.
 
Back
Top Bottom