Kuna nini Utumishi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna nini Utumishi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mbogo31, Feb 1, 2012.

 1. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu nimeamua kuliza swali hilo kwa sababu nashindwa kufahamu nini tatizo katika idara hii nyeti kabisa ya serikali ambayo ndiyo inayotakiwa kutatua matatizo ya watumishi wa serikali. kama kuna mtu mwenye kuweza kufika sehemu hii naomba akafanye uchunguzi na kupata hasa sababu ni kitu gani!, je ni elimu za watumishi?, ni viburi vya hawa wakubwa wa idara hiyo? au ni dharau kwa watumishi wa serikali?, idara za utumishi kwa mfano wizara ya ulinzi, afya nina mifano wa watu kadhaa ambao wanapata shida kwa kutopata mishara yao kwa muda wa miezi sita, tisa na hata mwaka mzima, wakiuliza wanambiwa majina yao sijui hajaingia kwenye payroll mara system mbovu. (sytem mbovu mwezi, mwaka? system ipi? fukuza huyo IT)


  Hivi kweli kuna sababu gani za msingi kwa mtumishi kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupata mshahara, hivi hawa maofficer utumishi wanafanya kazi gani?, hivi wanafikiri kwa kutumia vichwa hawa?, sasa mtu hajapata mshahara mwaka mzima je anaishi vipi?, anakula nini, anavaa nini? nauli ya kwenda office anapata wapi? kama anasomesha je watoto watakwenda shule? kama amepanga si atafukuzwa kwenye nyumba? kweli hii ni serikali gani isiyojari watumishi wake!

  kwa hali hii huyu mtumishi atafanya kazi kwa moyo kweli, atakuwa na ufanisi unaotegemewa kweli? je akipewa rushwa atakataa na je kama hayo yote yakishindikana ataishi vipi? kama ni binti hajaolewa siatafanya mambo asiyopenda kufanya ili aishi? na kama ni kijana si atapata shugamami na hapo sindio balaa kwa jamii jamani.!!?

  Ndugu zangu mliopewa dhamana ya nchi hii fungueni macho nchi inanuka uoza na watu hawawajibiki ipasavyo, watu wangewajibika ipasavyo wala msingesikia migomo na wala msingekuwa mnawalaumu Chadema.

  Majina ya Watu wanaofuatilia Mishara kwa mwaka sasa yapo na hao maofficer utumishi majina yanajulikana na majibu yao kwa hawa watumishi wanyonge yanakatisha tamaa hata kuyaeleza.

  Nimeamua kuwasemea hawa wanyonge wanao nyanyasika kwa kunyimwa haki yao kwa makusudi kabisa na bila sababu za msingi.

  MWENYE KUWEZA KUFANYA UCHUNGUZI KWENYE HII IDARA NA AFANYE HALI NI MBAYA SANA TUTAKAA TUKILAUMU WATUMISHI HAWATUHUDUMII IPASAVYO KUMBE MTU ANAWAZA ATAKULA NINI NA NDIO MAANA UKIONGEA KWA HERUFI KUBWA UNAELEWEKA MARA MOJA.
   
Loading...