Kuna nini mbona hawa ndio wanampiga Lowassa!

Kuna nini mbona hawa ndio wanampiga Lowassa!

Tatizo ni pale ambapo mwizi napiga kelele sana kuhusu mwizi mwingine. Sio yeye tu anatumia kisingizo cha kuutumia umaskini kutuibia, yako wapi maisha bora kwa kila mtanzania. Au kati ya wale wanaoteua majina, naomba jina moja la ambaye si fisadi, au kati ya waliotia nia any possible candidate ambaye si fisadi.

My view is usafi is not an issue here. kama issue ni usafi CCM haina mgombea.

Mkuu ni kweli hakuna mgombea aliye msafi CCM lakini wanatofautiana levels za uchafu. Lowassa ni top kwenye hiyo list.

Tiba
 
ndugu kama hizi taarifa zako ni za ukweli nini kazi ya tis..pccb..police na wengine..kwa nini rais wako alie madarakani hamchukulii hatua lowasa kwa madai yote hayo!?...watu wanahangaika kumchafua lowasa lkb ndo kumbe mnazidi kumweka juu na watanzania wengi wanaliona hilo...wanaomchafua wanajua kabisa jamaa atawaharibia ndo mana mko bize kuleta mashtaka yasiyokua na kichwa wala miguu.

waacheni watanzania wenyewe wataamua kwenye sanduku la kura

Mkuu maswali yako ni magumu kuyatolea majibu, lakini jiulize kwani EPA, RICHMOND, DOWANS, IPTL, SONGAS, SYMBION, ESCROW, MEREMETA, MWANANCHI GOLD,DEEP GREEN, RADAR, kuuzwa kwa wanyama wetu hai huko Qatar etc TAKUKURU na TISS walikuwa wapi?
 
Pia sijamsikia Lowassa akimsema mtia watia nia wenzake vibaya ila baadhi yao ndio wanamuandama.
 
Wewe tukana kama unavyoweza lakini hatuwezi kumkabidhi nchi mtu ambaye ni mwizi. Unakumbuka suala la EPA lilipoibuliwa yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kusema hizo ni habari za kwenye mitandao hazina ukweli wowote. And do you remember what was the end result? Hatumtaki mwizi kuingia Ikulu period.

Tiba

et hatuwezk

wew kam nani?
 
Acheni unafki hizo pesa katumia wapi?
Kwenye kile kimin bus?
Pita mtaani ufanye research uje na statistics uoneshe wananchi waliotumika na hizo pesa.

Acha kuongea kitu usichokijua. Wewe kutokutana na hilo fungu la yeye kugawa pesa haimaanishi hajagawa pesa. Pesa zimetolewa sana kununua wadhamini. Na sehemu nyingine wajanja ndio wamekula kwa niaba yenu. Shahidi ni mimi mwenyewe.
 
jiulize? kwanini BUNGE LILISIMAMA KWA DK 1,JANA!!

WHY?

SIRI GANI WANAYOIFAHAMU WABUNGE?

WABUNGE WOTE NI WEHU MPAKA KUMSHANGILIA LOWASSA!

KWANINI PINDA NA WENGINE HAWAKUPIGIWA NDEREMO?

Nguvu ya pesa mjomba, Wahenga walisema penye udhia penyeza rupia. wewe unashangaa kwa lowasa kushangiliwa na wabunge wa CCM.? Kwani hujui kuwa 90% ya wabunge wa CCM ni wehu.?
 
mzee wa kismati

lowasa alisema naijua CCM.wanampinga kwa sababu anaijua ccm .vilivyo.huyo 6 ni m nafki mkubwa lililohujumu katiba ya Tanzania likawatukana viongozi was Dini.Leo linataka Urais fisadi hill lishwindwe
 
Last edited by a moderator:
Mtu yeyote anayechukia rushwa, anayejua ubaya wa Rostam Aziz, anayewajua akina Karamagi na vibaka wote wanaomzunguka Lowassa lazima atampiga Lowassa. CCM wanajuana siyo wajinga acha wampige Lowassa siyo wa kuchekea.
 
lowasa alisema naijua CCM.wanampinga kwa sababu anaijua ccm .vilivyo.huyo 6 ni m nafki mkubwa lililohujumu katiba ya Tanzania likawatukana viongozi was Dini.Leo linataka Urais fisadi hill lishwindwe
Huko kuijua CCM na kuwaibia bila aibu ndiyo sababu wanampiga. Ataenda ikulu kutuibia bila hiana kisa tu anaijua CCM, acha wamkate kieleweke.
 
Ndiyo naweza kuprove kuwa amegawa pesa. Na wewe unaweza kuprove kuwa hajagawa pesa, ama ndiyo bendera fuata upepo.?

Weka hapa huo ushaidi wa yeye kugawa cash, nimehudhuria mikutano yake sijaona mtu akipewa na wala myself sijapewa..mkubali tu jamaa nyotaaa! hili ni ZIMWI tulijualo mistake kutuletea ZIMWI tusilolijua. EL next president 2015 hutaki hama nchi au kula malimaoo!:hand:
 
Hivi kweli mtu anaweza kusakamwa na watu kila upande kama hana tatizo? tafakari
 
kusema ukweli mpenzi wa Mungu......sijaona mwanasiasa mvumilivu kama Lowasa,TUHUMA MBAYA NI YEYE,FISADI YEYE,MWIZI YEYE,KUNUNUA WATU YEYE,KUTAKA UONGOZI KWA NGUVU YEYE,KULIPIZA KISASI YEYE......? Hayo yote kama ni kweli Tusubiri maamuzi ya wakubwa ila kama mimi ndio ningekuwa EL ningekuwa nimeshakufa kwa pressure......Watanzania tupunguzeni mdomo ukweli utatuweka huru

nb....team Barcelona and yanga
 
Weka hapa huo ushaidi wa yeye kugawa cash, nimehudhuria mikutano yake sijaona mtu akipewa na wala myself sijapewa..mkubali tu jamaa nyotaaa! hili ni ZIMWI tulijualo mistake kutuletea ZIMWI tusilolijua. EL next president 2015 hutaki hama nchi au kula malimaoo!:hand:

Hivi kwa akili yako inavyokutuma unategemea watu waje na fuko la pesa siku ya mkutano na kuanza kuzigawa kwa raia kama njugu.? Haiyumkini umezidiwa kete na hao wagawa fungu. Next time try to be smart dude.

NB : Nilikuuiza kuwa una proof yoyote ambayo inaweza dhihirisha kuwa pesa hazijagawiwa.?
 
Back
Top Bottom