Kuna nini kinaendelea NHIF?

Kuna nini kinaendelea NHIF?

Mwaikibaki

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2015
Posts
3,047
Reaction score
3,775
Siku ya jana mfuko wa bima ya Taifa ya Afya alias NHIF walitoa taarifa ya kuanza kutoa huduma kwa kifurushi/kitita kipya kuanzia tar 1.3.2024. Taarifa hii ilitolewa na Mkurugenzi wake.

Jana hiyo hiyo Chama cha Wenye Hospitali Binafsi (APHFTA), kikatangaza tena kugomea kuwahudumia Wanachama wa NHIF wakisema kuwa watapata hasara na hatimaye kufunga kutoa huduma.

Hapa sielewi kipi kinaendelea, hivi NHIF hii michango yetu tunayokatwa au tuliyolipa kwa ridhaa kwa sekta binafsi inaenda wapi maana ni muda sasa za chini chini zinaonyesha mfuko una hali mbaya kifedha, kwa hali hii issue ya universal health coverage aka Afya kwa wote tutaweza kweli?

Mwenye kufahamu shida nini tusaidiane kuelewa maana ni kama sarakasi zimekua nyingi.
 
Back
Top Bottom