Loading failed
JF-Expert Member
- Sep 14, 2023
- 1,969
- 5,919
Mnasingizia nguvu za giza siyo kweli moja ya sababu ni ugumu wa maisha, mtu aoe ataleaje familia kama walio oa na kuolewa wenyewe mambo yao hayaendi?Ndugu kwa masikitiko makubwa.
Ipo nguvu iliyopo mioyoni mwa wazazi wetu, ndugu, jamaa na marafiki na hata wazee wetu kabisa ya kumlazimisha mara kwa mara kijana aliyefika 30+ kuoa pasi na kupepesa macho upande wa pili
Utakuta kijana akienda kusalimia kwao ana lazimishwa kuoa mpaka anaona nyumbani ni kero kweli kweli, ndugu wana mshambulia , dada zake ndiyo usiseme anakaliwa kakikao kabisa wakidai ni lini utatuketea wifi, wazazi wataseme unataka tufe ndiyo uoe kwa kweli hili jambo ni gumu sana.
Hii nguvu ukiifatilia sana haina tofauti na nguvu za uharibifu unamsukuma kijana kuoa,unamjaza stress na presha juu unatarajia nini si nikumuangamiza huku kwa makusudi kabisa.
Hebu njoeni mseme wenyewe kwa hawa wanawake wasasa hawa wazee na ndugu zetu wanatuchukuliaje sisi vijana wa 30+ ambao hatujaoa
Weka hapa watu wapate uzoefuMimi niliwapa jibu moja mpaka leo sijaulizwa hilo swali tena, maana walianza hadi kutaka kunitafutia
Lipi mkuu?Mimi niliwapa jibu moja mpaka leo sijaulizwa hilo swali tena, maana walianza hadi kutaka kunitafutia
Mkuu,Wengine Huwa wameshawekwa wakfu kwenye madhabahu ya uchawi tokea wakiwa matumbuni mwa mama zao mfano waje kuzaa watoto watakaorithishwa uchawi.
Ukiona mzazi anauchagulia mke/Mme jiulize swali kwamba ana maslahi yapi kwa mke/Mme huyo?
Dunia Hii Babaa LukumbalukumbaMnasingizia nguvu za giza siyo kweli moja ya sababu ni ugumu wa maisha, mtu aoe ataleaje familia kama walio oa na kuolewa wenyewe mambo yao hayaendi?
- Usiku kucha wajasiliamali na wafanya biashara wanalalamika biashara haziendi na baadhi wako humu wanatafuta waganga wakuwatengenezea nyotta
- Watumishi wa umma ndiyo hao wanachangishana vikoba huko still maisha hayaendi madeni lukuki, vitu vimepanda bei vipato haviongezeki
- Wakulima nao wanazalisha masoko yakipatikana wanapangiwa bei kandamizi na wapi wauze bidhaa na wapi wasipeleke hata kama bei ni nzuri.
- Wageni wanachukua nafasi za ajira ambazo zingefanywa na hao wanaolalamikiwa kutooa,