Kuna muda huwa nashindwa kabisa kuwaelewa Waafrika dhidi ya Marais wao waliowaumiza na kuwaongezea Umasikini mkubwa walionao sasa (leo)

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Hivi Rais kama Idriss Deby wa Chad ( sasa Marehemu ) Kwanza amedumu Madarakani kwa miaka 30, Katesa na Kuua sana Watu, Kaharibu Demokrasia nzima ya Chad, kazaa na Wake za Wateule wake, alikuwa Mkabila na Mdini, kapendelea mno Kwao, wala hakujali Wafanyakazi wake kwa Kuwaongezea Mishahara yao, kaharibu Uchumi, Umoja, Ustawi na Mshikamano wa Chad leo Kafa Wananchi hao hao wa Chad 'Wanamlilia' na mpaka kupewa 'Maziko' ya Heshima na Makubwa.

Sijui ni nani 'Katuroga' hivi Sisi Miafrika!!
 
Bado hatujawa tayari kuwa viongozi wa waafrika wenzetu, ilipaswa tuendelee kuwa chini ya wakoloni.
 
Huyo dikteta wa chad katawala miaka 30/5 na akayafanya yote hayo aliyoyafanya.
 
Ingekuwa kuuwa watu ni Kinga ya kifo naamini watawala wa kiafrica wangeishi milele.
Maana mtu mwenye akili timamu hawezi ua mtu hali nae ni marehemu mtarajiwa labda tu kama ni luciferous yaani muabudu shetani so uwatoa kafara watu kwa mungu wao.
 
Mbona hushangai hata Rais wa Ufaransa nae kaenda kujiliza huko wakati wao Wazungu ndio wanatuambia wanajua vizuri kuutambua utawala bora au udikteta wa Muafrika!?!
 
Hivi Rais kama Idriss Deby wa Chad ( sasa Marehemu ) Kwanza amedumu Madarakani kwa miaka 30, Katesa na Kuua sana Watu, Kaharibu Demokrasia nzima ya Chad, kazaa na Wake za Wateule wake, alikuwa Mkabila na Mdini, kapendelea mno Kwao, wala hakujali Wafanyakazi wake kwa Kuwaongezea Mishahara yao, kaharibu Uchumi, Umoja, Ustawi na Mshikamano wa Chad leo Kafa Wananchi hao hao wa Chad 'Wanamlilia' na mpaka kupewa 'Maziko' ya Heshima na Makubwa.

Sijui ni nani 'Katuroga' hivi Sisi Miafrika!!
Cult personality, propaganda, and brain washing is the reason.

Mtu anaweza kumpenda mtawala kwasababu anatukana wazungu, ni mtu wa kabila au dini yake, wanatoka sehemu moja, au anawasomesha namba watu fulani.

Au huyo mtawala kampa hata 5,000 mwingine hakutoa

Au watu wanaoshindana na huyo mtu hawapendi.
 
Hivi Rais kama Idriss Deby wa Chad ( sasa Marehemu ) Kwanza amedumu Madarakani kwa miaka 30, Katesa na Kuua sana Watu, Kaharibu Demokrasia nzima ya Chad, kazaa na Wake za Wateule wake, alikuwa Mkabila na Mdini, kapendelea mno Kwao, wala hakujali Wafanyakazi wake kwa Kuwaongezea Mishahara yao, kaharibu Uchumi, Umoja, Ustawi na Mshikamano wa Chad leo Kafa Wananchi hao hao wa Chad 'Wanamlilia' na mpaka kupewa 'Maziko' ya Heshima na Makubwa.

Sijui ni nani 'Katuroga' hivi Sisi Miafrika!!
Waafrika watanzania idris deby jiwe miaka 30 5/6 chad bongo wake za wateuliwa wake za wateuliwa na mashemeji...oh kumekucha tayari saa mbili na nusu!
 
Hivi Rais kama Idriss Deby wa Chad ( sasa Marehemu ) Kwanza amedumu Madarakani kwa miaka 30, Katesa na Kuua sana Watu, Kaharibu Demokrasia nzima ya Chad,
Unaharibu vipi kitu ambacho haki-exist?! Ukiisoma historia ya Chad, tangu kupata uhuru wake ile nchi imekuwa ni full matatizo! Rais aliyekuwa ameondolewa madarakani na Deby, ni miaka michache iliyopita tu mahakama ya uhalifu wa kivita ilimtia hatiani kwa mauaji ya zaidi ya watu 40K! Sasa hapo unaamini Deby aliichukua nchi iliyokuwa na demokrasia?

Tatizo kubwa la Chad ni vikundi vya uasi vya ndani, na hii sidhani kama ni sahihi kumlaumu Deby kwa sababu ni migogoro ya waasi ilianza yangu miaka ya 60, na iliendelea kwa karibu miaka 15. Mara tu baada ya mgogoro huu wa ndani kwisha, hapo hapo ukaibuka mgogoro wa vikundi vingine vya waasi waliokuwa wanatokea Libya. Mgogoro huu uliendelea kwa takribani miaka 10 hadi Ufaransa ilipomwingiza madarakani rais ambae ndie alikuja kupinduliwa na Deby. Huyu Rais wa "Ufaransa" inaelekea alikuwa na hasira sana na waasi, kwahiyo aliua watu vibaya mno hadi alipokuja kuondolewa madarakani na Deby. Deby mwenyewe ile anaingia tu madarakani, vikundi vya uasi wa ndani vikaanza tena, zikapigwa hapo kwa miaka kadhaa. Uasi wa ndani ulipoanza kupumulia mashine, vikazuka tena vikundi vya kigaidi kutokea Libya bila kusahau Boko Haram.

Haya sasa, hivi hapo kuna demokrasia iliyokuwa imeharibiwa na Deby? Sana sana yeye ndo ALIJIFANYA kuleta hiyo demokrasia lakini kama ilivyo dasturi ya Miafrika, huku ile ya Afrika Magharibi ikiwa too much, demokrasia aliyojifanya kuileta haikuwa demokrasia. Na Afrika hakuna nchi ngumu kuiongoza kama ile yenye ratio inayokaribiana ya Wakristo na Waislamu au nchi yenye makabila makubwa mawili, ingawaje ni ugumu unaoletwa na viongozi wenyewe. Hata ukiangalia Chad, ni rais wa kwanza wa nchi hiyo tunaweza kusema ndie chanzo cha yote kwa sababu alipoingia tu madarakani, utawala wake ukaanza kuyatenga makundi mengine ya Chad, na hapo ndipo balaa lilipozuka, na halijaisha hadi kesho!!
 
Hivi Rais kama Idriss Deby wa Chad ( sasa Marehemu ) Kwanza amedumu Madarakani kwa miaka 30, Katesa na Kuua sana Watu, Kaharibu Demokrasia nzima ya Chad, kazaa na Wake za Wateule wake, alikuwa Mkabila na Mdini, kapendelea mno Kwao, wala hakujali Wafanyakazi wake kwa Kuwaongezea Mishahara yao, kaharibu Uchumi, Umoja, Ustawi na Mshikamano wa Chad leo Kafa Wananchi hao hao wa Chad 'Wanamlilia' na mpaka kupewa 'Maziko' ya Heshima na Makubwa.

Sijui ni nani 'Katuroga' hivi Sisi Miafrika!!
Hivi Rais kama Idriss Deby wa Chad ( sasa Marehemu ) Kwanza amedumu Madarakani kwa miaka 30, Katesa na Kuua sana Watu, Kaharibu Demokrasia nzima ya Chad, kazaa na Wake za Wateule wake, alikuwa Mkabila na Mdini, kapendelea mno Kwao, wala hakujali Wafanyakazi wake kwa Kuwaongezea Mishahara yao, kaharibu Uchumi, Umoja, Ustawi na Mshikamano wa Chad leo Kafa Wananchi hao hao wa Chad 'Wanamlilia' na mpaka kupewa 'Maziko' ya Heshima na Makubwa.

Sijui ni nani 'Katuroga' hivi Sisi Miafrika!!

Tatizo lipo kwa wananchi , tumekuwa vilaza mno kwa kuwa na akili za kupachikiwa na mzungu , mfano hoja zako kwa mtu mwenye utimamu anagundua kuwa umelewa propaganda za magharibi , wazungu wanapenyeza waas ktk taswira ya raia hlf serikali ikiwazibit vzr ndo wazungu wanakuja juu eti serikali imeua raia wema mf Ethiopia , UN inasema jeshi la ethiopia linaua raia wkt kwny uwanja wa mpambano hawapo , nyumbu wanakubali ila wanaojielewa tunajua hii ni vita ya propaganda , pili Unadai mishahara iongezwe , hv unahisi , kiongoz ni bora aachie ela mtaan kwa kuongeza mishahara kila uchwao na thaman ya ela ishuke au ni bora alinde thaman ya ela kwa kumantain gharama za kimaisha ? Wazung wametulevya vibaya sana waafrika kwa kuamin kuwa tunapaswa kuwadiscuss vibaya tu viongoz wetu na kuzisifu serikali zao zinazoibagua na kuinyanyapaa jamii yetu ya watu weusi
 
Back
Top Bottom