TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Leo Mwenyekiti mtendi wa ACACIA duniani Professa John L.Thornton amewatoa taulo viongozi wa chadema wa wakiongozwa na bwana Tundu Lissu baada ya kukuabali kutulipa kodi zote zinazofikia Trilion 100 pamoja na gharama nyingine badala ya kwenda mahakamani kuishtaki Tanzania katika mahakama za kimataifa za biashara kama vile Tundu Lissu alivyokua anawadanganya wafuasi wake kua Tanzania itashtakiwa na ACACIA kwa kuvunja mkataba.
Hii imedhihirisha jinsi chadema inavyotumia nguvu kubwa kupotosha wananchi wengi katika mambo mengi ukiachilia mbali hili la mchanga.
Chadema na Lissu (Advocate Tumbo) walishapoteza uhalali wao wa kusema ukweli tangu mwaka 2015 kwa hatua yao ya kumpokea fisadi na sasa wanaendeleza mbinu zile zile za uongo na ghiliba kupotosha wananchi.
MUNGU hamfichi mnafki leo hii chadema na Lissu wameumbuka mchana kweupe yale waliyowadangaya na kuwatisha Watanzania yamepingwa vikali na Mwenyekiti huyo wa ACACIA kwa kusema kampuni hiyo haitoishtaki Tanzania badala yake italipa deni na kujenga kiwanda cha kuchenjulia dhahabu (Smelter) hapa hapa nchini kitakachotoa ajira kwa maelfu ya vijana wa kitanzania.
Katika hili Mh Magufuli ametengeneza faida mara mbili kwanza amewezesha nchi kupata fedha nyingi kwa mara moja na pili amewezesha upatikanaji wa ajira kupitia kiwanda hicho kitakachojengwa na ACACIA hivyo kutekeleza ile ahadi ya ujenzi wa uchumi wa Tanzania ya viwanda kwa vitendo.
Tuendelee kumuunga mkono Rais Magufuli katika ujenzi wa Tanzania mpya isiyo na ufisadi ,rushwa ,ukwepaji kodi ,uhujumu uchumi na unyonyaji.
Augustino Chiwinga.