Kuna MTU anataka msaada Wa haraka

comesucces

Senior Member
Feb 21, 2017
160
105
Jamani nilitaka nisahau salamu
Asalaam alykum !

Kuna MTU kakata tamaa ya maisha maana kila jambo analofanya haliendi na inafika kipindi anakosa hadi hela ya kula inamlazimu kuazima Pesa kutoka kwa ndugu zake lakini cha ajabu wanamtumia elfutano au hata wasimtumie sasa alikuwa anaomba ushauri kwangu hapo nimejitahidi kumtia moyo na kumfariji lakini phycologicay naona kashakata tamaa maana hadi anataka ajitose kwa waganga ushauri wenu juu ya fursa anayoweza kuifanya
 
Inaelekea huyu ndugu amezidiwa na msongo wa mawazo (stress)
Kwenda kwa waganga kutamfanya ajitumbukize kwenye shimo ambalo itakuwa vigumu kujitoa hapo baadaye.

Mshauri afanye mambo haya:
- Kwanza inabidi ajenge tabia ya kujitegemea badala ya kusubiri kutumiwa hizo elfu tano tano kutoka kwa ndugu.
Atafute huduma (service) ambayo ataweza kuifanya hapo anapoishi na kulipwa kwa siku au kwa wiki. Mfano kufundisha 'Tuition' mtoto/watoto wa shule ya msingi, kazi ya kusafisha mahali n.k

- Akishapata pesa kidogo aushughulikie mwili wake kwanza ili uwe katika hali nzuri na afya bora.
Hii itamuwezesha kichwa chake kufikiri vizuri na kupata njia bora zaidi za kujikwamua kiuchumi.
Ahakikishe anakula chakula chenye virutubisho bora (matunda na mboga za majani kwa wingi) na pia kunywa maji ya kutosha.

- Afanye mazoezi ya viungo mara kwa mara. Anaweza kufanyia nyumbani (sio lazima aende Gym)

Ni matumaini yangu kuwa atajitia nguvu na kutokata tamaa maana waswahili husema
'Kila penye maisha kuna matumaini!'
 
nice comment thanks for you
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom