El Roi
JF-Expert Member
- May 29, 2020
- 297
- 537
Kama nakumbuka vizuri wakati Lissu anatoa hotuba ya kukubali uteuzi wa kuwa mgombea kupitia chama chake alisema Mambo ambayo nina Shaka Kama yamefahamika kwa Chadema wenyewe au sisi wengine.
Kwanza aliomba tuondoe notion ya kila wakati wagombea kuja na ahadi kwa lugha rahisi ilani ya Mambo gani watayafanya. Kuna ukweli mkubwa hapo. Maana yake suala la tunahitaji Nini Hilo hata bila kuwa na ilani iliyoandikwa nionavyo ni Mambo yanayojulikana tu(naturally known) nani hajui kwamba vijiji vyetu vinahitaji maji, zahanati, na kwamba wananchi lazima wapate huduma za Jamii? Maana frankly speaking jukumu la serikali yoyote ni kutoa huduma za Jamii toshelevu.
Barabara, miundo mbinu ya elimu, afya, ulizi na usalama nk haya ni Mambo ambayo hata mwananchi wa kawaida anajua serikali inapaswa kuyafanya maana ndo kazi zake hizo kwa asili.
Jambo zito ambalo nadhani pamoja na kuelezea ilani kwa maana ambayo serikali inayotafuta kuchaguliwa itafanya, ni vizuri kujua Mambo muhimu au mfumo wa kufanya Mambo hayo yatokee kwa urahisi na yawe na maana.
1) Katiba inayokwenda na wakati na kujumuisha matakwa ya wakati, nadhani Ni Jambo tunalohitaji Sana na litakaloharakisha maendeleo ya Jamii yetu. Jambo ambalo silijui kwa hakika Ni Kama watanzania wanaona uzito wa ajenda ya Lissu. Kwa sababu ya mazoea ya kuzifanya ilani kuwa ni suala la kuhaihidi hicho kinachoitwa huduma za Jamii, maji umeme,hospital nk Kuna hatari mgombea huyu kuonekana Hana ajenda. Lakini ukweli wa Mambo ni kwamba ni vigumu sana kupata maendeleo ya Sasa wakati mifumo, Sheria, taratibu unazotumia zikiwa zimepitwa na wakati.
Ni Kama methali ile ya zamani ya kutaka kuweka divai mpya kwenye kiriba kikuukuu. Ukiweka divai mpya kwenye chombo kizee hicho chombo kitapasuka hakika.Maendeleo ya kisasa hayatawezekana hakika wakati mifumo ya kuendesha Mambo bado ni ya kizamani. Napenda Sana falisafa ya Tanzania mpya. Ni Jambo la kweli, lakini ukweli ni kwamba lazima kuwe na ku-streamline, mifumo, Sheria na hata miundo ya Mambo kadhaa ili kuyafikia hayo mapya.
2) Miundo wa utawala, bado ni Jambo la kuangalia Sana na ukweli hii Ni ajenda ya muhimu Sana. Dhana ya kugatua madaraka(Devolution and not Decentralization) ndo injini ya maendeleo. Muundo wetu wa utawala mantically speaking,unachelewesha maendeleo. Ugatuzi kwa maana ya Devolution Kama ilivyo kenya kwa kuanzia, ndo njia yenye ufanisi ya utawala itayoharakisha maendeleo ya jamii.
Lundo la viongozi wa kuteuliwa waliojaa ngazi za chini za utawala mikoa, wilaya nk hawawezi kuleta maendeleo ya haraka kwa sababu hawawajibiki moja kwa moja kwa wananchi. Lakini kama hakujawa na centre za huduma za karibu za watu, hayo maendeleo utayapata lini na muda gani kwa haraka?
Governor ambaye kawekwa na wananchi na ana bajeti yake hatashindwa kujua mahitaji halisi ya watu wake na hivyo kuwapa huduma zinazotakiwa. Maana kiuhalisia anayaona mahitaji yao kwa karibu na ana pesa za kibajeti za kumfanya awape wananchi maendeleo yao.
Ugatuwaji kamili (Devolution) wa utawala na siyo Decentralization kama ilivyo sasa ndo tunalohitaji ili kusukuma maendeleo kwa hakika na kwa haraka. Wasiwasi wa kudhani nchi itagawanyika na mengineyo ni hofu tu ya kutufanya tusifanye mambo ya wakati kwa wakati. Kumbuka kile unachoogopa kitakushinda(what you can't defeat will definitely defeat you).
Katiba mpya na muundo mpya wa utawala ni Mambo ambayo mie nayaona kama vyombo vya kutufikisha/kutubeba kutupeleka kwenye Mambo makubwa na Tanzania mpya tunayoihitaji. Hapa ndo wasiwasi wangu unapokuja je Lissu anaeleweka? Au aje tu na traditional ways of asking for votes? Nitaleta maji, nitajenga mashule, nitatoa elimu bure, nk.
Hata hivyo kipya ni kipi hapo ?maana upende usipende kwa kuwa kuwa tu unatafuta kuongoza watu, hayo Mambo utayafanya. Swali ni je, kuna mifumo sahihi ya kuleta into reality hayo yanayoitwa maendeleoYa watu na hata hayo ya vitu? I sympathize with you Lissu maana inawezekana unashughulika na Jamii iliyozoea kuaihidiwa badala ya Jamii inayoshabikia mifumo inayoleta matokeo haraka na kwa uhalisia.
Najua kwa kuwa unatafuta kura utaahidi lakini nakusihi usiache kusemea Mambo ya msingi Kama haya ambayo kwetu wengine tunaona ndo agenda kubwa za uchaguzi (major topic) na ahadi za huduma za Jamii ni sub topic.
Wasalaam