Kuna msemo wa kifalsafa wa kichina.( 当该国处于战争状态时,醉酒者和妓女继续在酒吧和赌场酗酒并发生性关系。)

Kuna msemo wa kifalsafa wa kichina.( 当该国处于战争状态时,醉酒者和妓女继续在酒吧和赌场酗酒并发生性关系。)

mr mkiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
5,727
Reaction score
11,952
Maana yake "Taifa linapokuwa katika hali ya vita, walevi na machangudoa huendelea kunywa na kufanya ngono kwenye mabaa na makasino"

Katika mantiki ya kifalsafa msemo huu hauwahusu walevi wa pombe na wafanya biashara ya ngono, hapana; bali wananchi wasiojua wanachokifanya kwa ajili ya nchi yao (walevi) na wananchi wanaofanya mambo yasio na maana wala faida kwa taifa bila kujali yanayoendelea.

Hali ya vita iliyotajwa hapo sio lazima iwe vita ya kuvamiwa kwa silaha maadui wa nje. No, inaweza kuwa jambo lolote linalohitaji kupigiwa kelele na kufanyiwa maamuzi ya haraka kwa faida ya Taifa zima; ingawa msemo wenyewe ukitumika wakati wa vita ya China na Japan (Sino-Japanese war) ya mwaka1937.

Walevi na Machangudoa, ndio watu wasio na msaada wakati wa vita kama wakiendelea na matendo yao hayo. Hao ndio wanaopiga kelele kutetea vitendo vya kuteka watu, na majaribio ya mauaji. Ndio hao wanaotukana maaskofu na wanaharakati wanaopinga uovu wa serikali. Hao ndio watu wa kwanza kukimbia nchi itakapongia katika machafuko.
Vijana wanaopinga maovu ya serikali wakati ambao maisha ya wapinzani hayana thamani, ndio hasa wanajeshi halisi. Kwa kuwa uzalendo ni kuipenda nchi, sio lazima serikali. Wakati mwengine serikali hushikwa na kundi la waasi, au wahuni au matapeli. Lakini nchi ipo tu. Kupinga uovu wa serikali ni ishara ya uzalendo, kiashiria cha tamaa ya mabadiliko chanya kwa nchi. Wanaochukia uzalendo huu ni Walevi na Machangudoa.

Jumapili ya Tarehe 25 machi 2018 ilikuwa jumapili ya Matawi kwa imani za kikatoliki. Huko Vatican, Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis aliwataka vijana kupaza sauti dhidi ya wazee wanaofanya ndivyo sivyo. Aliwataka vijana wasilale badala yake waongoze mapambano, kuwakosoa na kuwapinga 'wazee' wanaotenda kinyume na taratibu. Vijana waliokuwepo katika misa ile waliitika kwa sauti kubwa kukubaliana na Papa Francis.
Sio wakati wa kulala. Bahati nzuri wapo wazee ambao wanafikiri kama vijana. Tumeona hatua za maaskofu wa KKKT na TEC. Nyaraka zao ni sehemu ndogo ya harakati zinazotakiwa kwa sasa. Lakini kwa bahati mbaya kuna vijana wanafikiri kama wazee, ambao hawataki kujadili yaliyomo kwenye nyaraka hizo badala yake wanazusha propaganda na uongo ilimradi kutetea ugali wao. Hao ndio walevi na machangudoa wetu katika harakati.

Ni wakati sasa wa kuungana
na Maaskofu wetu kwa kauli moja. Muunganiko huu ukaondoe ile dhana ya upinzani kwa mslahi ya kisiasa. Maaskofu hawana maslahi yoyote ya kisiasa lakini wamesikia na kuona mateso wanayopata kondoo wao, wamepaza sauti.

Na sasa, harakati hizi sio za chama fulani dhidi ya chama kingine. Sio upande huu na ule. Bali ni upinzani wa wenye akili dhidi ya wajinga. Wema dhidi ya uovu. Uzalendo dhidi ya ulevi na uchangudoa wa kisiasa.
Tusome na kurudia rudia na kutafakari nyaraka za maaskofu.

Tusikae kimya.

mr mkiki.
 
Back
Top Bottom