Kuna mambo mengi yanazungumzwa mitandaoni kuhusu uchaguzi wa jana wa EALA

PRODA LTD

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
1,005
1,333
Nimetoa kwenye ukurasa wa Facebook wa Malisa GJ.
Kuna mambo mengi yanazungumzwa mitandaoni kuhusu uchaguzi wa jana wa EALA. Sikutaka kutoa maoni yangu lakini ngoja niseme yafuatayo;

Kitendo cha Kamati kuu ya chama chetu kuwapitisha wagombea 6 maana yake iliwaamini hao 6 kati ya wengi waliochukua fomu. Na sisi wanachama tulikua tayari kumpokea yeyote kati ya hao 6 ambaye angechaguliwa. Wote 6 walionekana wana sifa, wote 6 walionekana kuwa na uwezo, wote 6 walionekana wanaweza kuwakilisha taifa.

Yeyote kati ya hao 6 angepita itz fine maana amechujwa na kuaminiwa ndani ya chama. Kama kuna ambaye hakua na uwezo hakutakiwa kupitishwa. Lakini kama chama kimewapitisha means kimeona wote wana uwezo.

Sasa hizi kelele za kulalamika zinatoka wapi? Mlitaka nani achaguliwe na nani asichaguliwe? Kama kuna ambaye hamkutaka achaguliwe kwanini mlimpitisha ndani ya chama? Kabla hamjalaumu bunge kuchagua hao ambao "mlikua hamuwamtaki" mnapaswa kukilaumu kwanza chama kwa kupitisha "watu msiowataka". Lakini kama chama kilifanya uteuzi na mkaona wote wanafaa, inakuaje baada ya uchaguzi mnaona kuna ambao hawafai?? Unafiki.!!

Mimi binafsi nilikua na imani na yeyote kati ya wagombea 6 waliopitishwa. Wapo wengine wengi waliochukua fomu na walikua na sifa lakini chama kikapitisha 6 tu. So yeyote kati ya hao 6 angeshinda itz okay, as long as ni mtu aliyeaminiwa na chama, akachujwa na kupitishwa.

Wangechaguliwa mwanamke mmoja na mwanaume mmoja ni sawa. Wangechaguliwa wanaume wote ni sawa (maana EALA sio TAMWA), wangechaguliwa wanawake pia wote ni sawa. Vyovyote ambavyo ingekua ni sahihi maana ni matakwa ya demokrasia.

So tulipopeleka majina bungeni tulipaswa kujua lolote linaweza kutokea. Ama mwanamke na mwanaume, ama wanaume wote, ama wanawake wote. Hiyo ndiyo demokrasia. Kitendo cha kusema kuwa wabunge walipaswa kuchagua mwanaume mmoja na mwanamke mmoja, ni kuingilia demokrasia ya bunge. MSIWAPANGIE.!!

Kuna watu wanatoa hoja kuwa wanawake hawakujieleza vizuri sana. Hii ni hoja mufilisi kabisa. Unapimaje uwezo wa mtu kwa kuongea dakika 3?? Dakika 3 haziwezi kuwa kipimo cha competence ya mtu. Mwaka 1966 Joachim Chisano alipotaka kugombea uongozi ndani ya chama chake (FRELIMO) alipewa dakika 5 za kujieleza kwenye panel ya founders wa chama hicho na akaonekana mgombea wa hovyo kabisa kwa kushindwa kujieleza vizuri.

Lakini miaka 20 baadae alifanikiwa kuwaeleza watu wa Msumbini kwanini anafaa kuwa Rais wa taifa hilo na wakamchagua. Na akadeliver kwa kiasi kikubwa sana. Leo huwezi kuzungumzia historia ya marais bora wa Msumbiji ukaacha kumtaja Chisano. Lakini ni Chisano huyohuyo aliyeshindwa kujieleza ndani ya dakika 5 alipogombea uongozi wa vijana.

So dont get confused guys. Kupima uwezo wa mtu kwa dakika 3 sio kumtendea haki. However kuna wagombea wengine wamewahi kuwa wabunge, so wana experience na bunge, definatelly lazima watajieleza vizuri zaidi maana wana uzoefu. So kusema kuna wagombea hawezi kwa sababu wamejieleza kwa wasiwasi, while mnajua ni mara yao ya kwanza kusimama bungeni sio kuwatendea haki.

Subirini waliopitishwa waanze kutekeleza majukumu yao, ndipo muwapime kama wanaweza au hawawezi. Lakini kuanza kupiga ramli kuwa hawataweza kisa mmewapima kwa dakika 3 za kujieleza huo ni uzwazwa. Acheni kupiga ramli vijana. Mnasemaje hawawezi wakati hata kuapa bado? How can u evaluate someone before perfomance? Let them perform then u can evaluate. Vinginevyo ni ramli tu.

By the way nakiamini sana chama changu Chadema, naviamini vyombo vyote vya maamuzi ndani ya chama changu na ninaviheshimu pia. Naamini Kamati Kuu kupitisha wagombea 6 ilijua wote wana uwezo na yeyote kati yao anaweza kuwa mwakilishi mzuri wa taifa. Kwahiyo naheshimu maamuzi ya bunge kama nilivyoheshimu maamuzi ya Kamati kuu ya chama changu. Mungu ibariki Chadema, Mungu wabariki wabunge wateule wa EALA. Mungu ibariki Tanzania.!

Malisa GJ
 
Watu walitaka majina makali majina yanayofahamika majina majembe pasipo kujua hata hawa nao wana CV nzuri tu
 
Subirini waliopitishwa waanze kutekeleza majukumu yao, ndipo muwapime kama wanaweza au hawawezi. Lakini kuanza kupiga ramli kuwa hawataweza kisa mmewapima kwa dakika 3 za kujieleza huo ni uzwazwa. Acheni kupiga ramli vijana. Mnasemaje hawawezi wakati hata kuapa bado? How can u evaluate someone before perfomance? Let them perform then u can evaluate. Vinginevyo ni ramli tu.
 
Waungwe mkono wapewe support. Kama chama kina uwezo kiwafunde na kuwapa mbinu za kuwa wawakilishi bora wa nchi kwenye EALA. Wanatakiwa waweze kubalance maudhui ya umoja wa Africa Mashariki na maslahi ya Tanzania. Wasifikirie kwamba wanakwenda kuitetea Tanzania tu huko, ni jukumu lao kuwezesha shirikisho bora lipatikane. Wana vigezo vya kujenga umahiri kwenye majukumu yao mapya. ALL the best.
 
maneno ya mkosaji..wenje ndiio lilikuwa tumaini lenu..jipangeni upya. ukanda udini unawa cost..
 
Back
Top Bottom