Kuna madhara nikiacha ulabu ghafla

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Ndugu zangu wa JF
Niko kwenye hatua za mwisho kukamilisha kusudio langu la kucha pombe. Nimekuwa nikinywa pombe kwa karibu robo tatu ya umri wangu. Nilifikia hatua ya kunywa safari kama 30 hivi ndo naanza kusikia kidogo sasa napata nishai. Kuna kipindi nikahamia kwenye Konyagi. Nikawa napiga mpaka mizinga 3 ile mikubwa na bado kesho yake niko fresh. Lakini nikapata shida kwenye hii konyagi. Nilianza kutokuona vizuri! Doctor alinishauri niache ze konyagi. Nikaanza kutangatanga, mara leo grants kesho teachers mara ndovu nk nk! Sasa siku za hivi nikaanza kujiuliza je kuna sababu ya kuendelea kunywa! Sasa naona yule roho wa kuukana ulevi inazidi nguvu! So nimeanza zoezi la kuacha kunywa kilevi. Je kuna madhara nitapata nikiacha kunywa pombe kabisa?
Naomba ushauri wenu.
Eeka Mangi
 
Ama nimwone daktari

Ndugu yangu pole sana na pia hongera kwa kulipa kodi nyingi kwa muda mrefu. too bad kodi yako inaliwa na waroho.
Back to Topic: naweza kusema we ni mlevi (no offence intended).
Nianze kwa kukuuliza kuwa umewahi kujaribu kuacha kabla? if yes, mara ngapi? Ulijisikiaje?
Kama bado mara nyingi ukiacha mtu unakua unaumwa kabisa, kama una malaria kali, homa, kichefuchefu na kutapika, baadhi wanatetemeka na kushindwa kufanya kazi sawasawa, kushindwa ku-concentrate...yani kwa ujumla unajisikia hovyohovyo.
Una familia (mke)? Kama unae nae anakunywa? Bcoz ni muhimu sana katika uthubutu wako huu wenye manufaa kwako (japo kodi ndo hivo inapungua).
Kwa hatua uliyokwisha fikia nakushauri ndugu yangu umuone daktari, a psychiatrist to be specific. They are equiped with psychosocial knowledge na nadhani utabenefit sana kama utamhusisha mtaalam katika suala lako.
Na bahati nzuri kama drive ya kuacha inatoka kwako.
Unaweza kuniPM kama unahitaji my recommendation of a doc.
Happy Rehab.
 
Pombe ina magonjwa 60 kwa binadamu

MOJA ya vyanzo vinavyolipatia taifa mapato kupitia makusanyo ya kodi ni pombe.
Lakini pamoja na faida zote tunazozipata, ukweli unabaki palepale kwamba pombe ina athari katika maisha ya binadamu.

Mwanzoni mwa mwaka huu wataalamu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na madaktari wastaafu walikutana na wanahabari jijini Dar es Salaam na kuzungumzia juu ya mkutano utakaozungumzia athari za pombe katika jamii.

Mkutano huo unaotarajia kufanyika Jan 13 hadi 14 mwaka huu mkoani Arusha, utashirikisha nchi za Afrika Mashariki.

Watunga sheria na wataalamu wengine kutoka serikalini watahudhuria huku ujumbe wa mkutano huo ni: ‘Kilevi si bidhaa ya kawaida na ni kikwazo katika maendeleo.’

Mkurugenzi Msaidizi na Katibu wa Magonjwa yasiyoambukiza, Dk. Joseph Mbatia, kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anasema serikali ipo mbioni kutengeneza sera itakayohusu utumiaji wa pombe ili kupunguza athari zake katika jamii.

Dk. Mbatia anasema wamelazimika kutunga sera hizo baada ya kuona matatizo yanayotokana na pombe yanaongezeka kila kukicha.

Anasema kabla ya sera hizo kupitishwa watafanya utafiti katika maeneo mbalimbali ili kujua ni jinsi gani jamii inavyolichukulia suala la pombe na madhara yake.
“Mfano, katika vijiji vichache tulivyofanya utafiti, wananchi walikuwa wakijitetea kwamba pombe

imewasaidia kuendesha maisha yao…lakini ukweli ni kwamba pamoja na faida ambazo zimekuwa zikiorodheshwa, hasara ni nyingi kuliko faida.

“Kwa mfano, bima zimekuwa zikilipwa kutokana na ajali zinazosababishwa na kulewa kupita kiasi,” anasema Dk. Mbatia.

Anabainisha kwamba sera zitakazowekwa si katika kupiga vita biashara ya pombe na badala yake zitakuwa zikiangalia njia bora za matumizi yake na kwa wale wataoonekana wameshaathirika watawekewa utaratibu wa kupatiwa tiba.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kanda ya Afrika Mashariki ya ‘IOGT-NTO Movement’, ambao ni waandaaji wa mkutano huo, Gunnar Lundstrom, anasema bado kuna changamoto zinazolikabili taifa katika kupunguza athari za pombe.

Anasema changamoto hizo ni pamoja na pombe kupatikana kwa gharama nafuu na hivyo kusababisha watu kunywa kupindukia.
Tatizo lingine anasema ni pombe kuwa moja ya chanzo cha mapato nchini, jambo linalofanya serikali kushindwa kupiga marufuku.

Naye Daktari mstaafu, Maletnlema Tumsifu, anasema kuna jumla ya magonjwa 60 yanayosababishwa na unywaji wa pombe.
Anataja baadhi ya magonjwa hayo kuwa ni mfarakano katika familia, maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi, unene kupita kiasi, utapiamlo hasi, mimba kuharibika na kisukari.

Dk. Maletnlema anasema kuna madhara ya pombe ya aina mbili. Kwanza ni kuathirika kwaa mishipa ya fahamu mwilini kote kwa kupunguzwa uwezo na pili ni kuungua baadhi ya ogani za mwili hasa tumbo pindi mtu anapokunywa.

Anaeleza kwamba katika kuathirika mishipa ya fahamu kumetizamwa kwa hatua nne za wanywaji, hatua ya kwanza ni ile ya kuchangamka.
Hapa mtu hujisikia mzima zaidi ya kawaida, moyo unapiga haraka, tumbo linameng’enya chakula haraka na hamu ya chakula kuongezeka.

Hatua ya pili, mtu akiendelea kunywa anachanganyikiwa na kuzungumza sana, kukosa aibu, utu kubadilika, kutawala tabia za kimwili, hamu ya chakula kuongezeka na hapa ndipo watu wanaagiza nyama choma kwa wingi.

Mnywaji akiendelea kunywa pombe hucharuka kutokana na neva zake za ubongo kushindwa kumiliki mwili.
Mambo yote anayoyafanya hayana utaratibu kwani mnywaji huwa mkorofi.
Dk. huyo anasema mnywaji huwa mkorofi na anaongea maneno yasiyo na maana, baadhi ya wanywaji huchukulia hatua hii kama raha yao. Hapa kitu kinachojitokeza ni kupoteza hamu ya kula.

Hatua ya nne mtu akilewa kupita kiasi huwa hajijui na analala fofofo kutokana na kupoteza fahamu. Huenda akajikojolea au kutapika, inategemea na kiasi cha pombe alichokunywa.
Wakati kwa upande wa ogani, pombe huathiri zaidi viungo vinavyopata pombe nyingi kila wakati mtu akiwa anakunywa.

Mfano wa viungo hivyo ni mdomo, koo na tumbo, ambavyo vyenyewe hufikiwa na pombe nyingi mara mtu anapomeza.

Tumbo likiumia inaonekana kama maumivu ya tumbo, pengine kutapika na kuharisha. Lakini kutokana na utaratibu wa tumboni, lazima chakula chote pamoja na sumu au madawa vinavyonyonywa tumboni vipitie katika ini kuondoa sumu na vyakula visivyohitajika.

Na kwa sababu hii, pombe yote mtu anayokunywa hupita katika seli za ini na zinajaribu kuiondoa lakini nazo zinalewa chakari na baadhi zina kufa.
Ieleweke kwamba tukinywa kidogo seli chache zinakufa na tukinywa sana zinakufa seli nyingi

na nafasi yake inajazwa nyuzi nyuzi za kovu.
Ini huwa na mabilioni ya seli ambazo ni imara, hata mtu akinywa pombe nusu, seli zake bado

zitaendelea na maisha kama inafikia kikomo ini linashindwa kufanya kazi na kujikuta njia za nyongo na mishipa ya damu inaziba.
Kila ogani ya mwili inaumia kivyake, lakini tumbo na ini ni mifano wazi.



chanzo: https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/80412-pombe-ina-magonjwa-60-kwa-binadamu.html
 
Back
Top Bottom