Kuna kitu hakiendi sawa: Mkuu anapambana na umma?

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Kuna mambo ambayo yanaonyesha kuna kitu hakiendi sawa lakini kwa hulka zetu za kishabiki na kutofuatilia mambo ya msingi nchi hii hatujakiona.

Kwana maoni yangu mkuu ana tabia ya kutotaka kushindwa kwa kila jambo na ukimkosoa umeharibu maana atafanya zaidi hicho unachomkosoa ili aonekane kashinda.

Alipolalamikiwa mwanzoni style yake ya uongozi hasa kwenye style ya kufukuza watumishi na bomoa bomoa alijibu 'SAA NYINGINE KIKWATAKWATA MAMBO YANAENDA"

Watu walipopiga kelele sana style ya Makonda akiwa DC wa Kinondoni akamteua kuwa mkuu wa mkoa na akasema "MSIYEMTAKA KAJA"

Wabunge wa CCM wamelalamikia ubabe wa serikali na watendaji wake hadi wakatishia kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu akasema "MKIPIGA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NAYE NITARUDISHA JINA LAKE NA MSIPOMPITISHA NITALIVUNJA BUNGE"

Wananchi wamemlalamikia mkuu wa mkoa wa Arusha kwa kulifedhehesha taifa mbele ya wafadhiri akasema "SINA MPANGO WA KUMTUMBUA BALI KUMPANDISHA CHEO"

Kubwa kuliko zote katika pressure hii ya Makonda na vyeti mkuu amempa 'LIVE COVERAGE YA TV YA TAIFA KUADHIMISHA MWAKA MMOJA MADARAKANI'
 
Nahisi kitu flani hapa........ngoja nisubiri. Labda kweli kimatafutwa kisingizio
 
Na kwapia hekima ndio kitu cha bure anahitaji kusikiliza ushauri tu atapata hekima ya uongozi.lakini kwa mwendo huu atashidwa t
Japo aige kwa lowassa. dispite walimsema vibaya.. wakamtungia hafi nyimbo... lakin yuko kimya.
Unajua kukaa kimya ni jib tosha kwa mjinga
 
The way anavyoenenda na kauli anayotoa ... sijui kama atafikia hayo malengo. Maana anajenga uhasama.. ubaguz.. kati ya wananchi ... akiendelea hiv.. hali hii itakuja kuwa mbaya alaf aanze kuja kulaum mtu fulani
 
Back
Top Bottom