Kuna kila dalili Korea kaskazini kuvamiwa kijeshi!

alexelias

JF-Expert Member
Sep 1, 2017
2,032
3,198
Kwa nilivyomshuhudia Mattis akiongea hakika ni suala la muda tu hawa wamarekani watakinukisha huko rasi ya Korea.

Jamaa ameonesha dhahili alienda White house kupeleka mfumo watakaotumia kuishambulia Korea Kaskazini.

Binafsi naamini kelele za Korea Kaskazini ni sawa na za Saddam Hussein-mwisho mshindi atakuwa USA.
 
Sawa itavamiwa but to the expense of South Korea and Japan civilians who might get obliterated by DPRK missiles counter strikes. This is a ridiculous and uncalculated move by Gen Mattis. Mgogoro huu umedumu kwa miaka zaidi ya 50, watu wenye busara wengi tu hawakujaribu kulianzisha huko nyuma so ukawa freezed. Kumbuka there has never been a peace treaty between the two Koreans, technically they are still at war and this one will be much deadlier.
 
Kiduku atafanyiwa shambulizi la kushtukiza hamtaamini na atasahaulika jumla. Lengo ni kuondoa kabisa kizazi cha Kim katika utawala wa NK. Sikilizia wanachi wa NK watakavyoshangilia baada ya dikteta kuondolewa. Wapate japo ahueni maana wameishi kama watumwa ndani ya nchi yao wenyewe wakati wenzao SK kama peponi vile.
 
Sawa itavamiwa but to the expense of South Korea and Japan civilians who might get obliterated by DPRK missiles counter strikes. This is a ridiculous and uncalculated move by Gen Mattis. Mgogoro huu umedumu kwa miaka zaidi ya 50, watu wenye busara wengi tu hawakujaribu kulianzisha huko nyuma so ukawa freezed. Kumbuka there has never been a peace treaty between the two Koreans, technically they are still at war and this one will be much deadlier.

Uzi huu wengi wanaousoma ni waswahilii tu, sasa unapotumia kiingereza nawafanya wengine wasikuelewe, jivunie lugha yako ya kiswahili.
 
Kwa nilivyomshuhudia Mattis akiongea hakika ni suala la mda tu hawa waMarekani watakinukisha huko rasi ya Korea.

Jamaa ameonesha dhahili alienda Whitehouse kupeleka mfumo watakaotumia kuishambulia Korea kaskazini.

Binafsi naamini kelele za Korea kaskazini ni sawa na za Saddam Hussein-mwisho mshindi atakuwa USA.

Tukumbuke pia Urusi hawana mahusiano mazuri na marekani, je unadhani warusi watamuunga mkono marekani? ni ngumu sana.
 
Sioni vita ikitokea hivi karibuni.
USA anajua kuwa anao uwezo wa kumpiga North Korea lakini hautakuwa ushindi rahisi na mwepesi bila kuacha kovu.
Nafasi za South Korea na Japan ni swala tete zaidi, damage kubwa itatokea kwenye nchi hizi na hazipo tayari kwa hilo au woga wa kutumika kwa silaha za maangamizi.
Dunia itaathirika vibaya sana kwa vita hii. Sioni ulimwengu ulio tayari kwa msukosuko mwingine mkubwa.
Note: Vita haina macho wala haichagui wa kumuathiri.
 
Lakini kuna kitu huyu dogo anakitafuta,kwani akikaa kimya bila ya kurusha hayo makombora atakosa nini,nadhani anatumia kiasi flani cha ulevi unaomfanya ajiamini na kuona kuwa yuko salama sana.Vita sio kitu cha kuombea,utaharibu uchumi wako,utawaweka watu wako katika maisha yenye mashaka muda wote,vifo vya raia visivyo na sababu n.k.,n.k. au hana TV inayomuonyesha yale magofu kule Syria...!
 
.
Kwa nilivyomshuhudia Mattis akiongea hakika ni suala la mda tu hawa waMarekani watakinukisha huko rasi ya Korea.

Jamaa ameonesha dhahili alienda Whitehouse kupeleka mfumo watakaotumia kuishambulia Korea kaskazini.

Binafsi naamini kelele za Korea kaskazini ni sawa na za Saddam Hussein-mwisho mshindi atakuwa USA.
Hapo nategeme makombora yasiyopungua 100000 kwa wakati mmoja kwa target tofauti ikiwemo vyanzo vya nishati, mawasiliano ya radio, TV, internet, Viwanja vya ndege, bandari, kambi za jeshi
N.k
 
Lakini kuna kitu huyu dogo anakitafuta,kwani akikaa kimya bila ya kurusha hayo makombora atakosa nini,nadhani anatumia kiasi flani cha ulevi unaomfanya ajiamini na kuona kuwa yuko salama sana.Vita sio kitu cha kuombea,utaharibu uchumi wako,utawaweka watu wako katika maisha yenye mashaka muda wote,vifo vya raia visivyo na sababu n.k.,n.k. au hana TV inayomuonyesha yale magofu kule Syria...!
Na USA akikaa kwake bila kufanya mazoezi ya pamoja na south mpakani atakosa nini ,

Mwaka Jana USA na south walivyofanya mazoezi ya pamoja dogo akajibu kwa kutest hydrogen na kurusha missile ,juzi makamanda 17500 wa USA na 50,000 walifanya mazoezi mpakani dogo akajibu kwa kurusha kombora anga la Japan

Kwa unavyohisi nani mkorofi ?

Hivi mfano Leo hii USA waje kufanya mazoezi ya pamoja na Malawi mpakani na Tanzania wewe utahisi nini

Kwanza muambie USA atoe pua lake kwenye rasi ile
 
Back
Top Bottom