Kuna jambo haliko sawa kuhusu magonjwa ya kudumu

Kuna jambo haliko sawa kuhusu magonjwa ya kudumu

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,709
Reaction score
19,558
Mtakubaliana na mimi sasa hivi katika nchi yetu kuna mlipuko wa kushangaza sana wa magonjwa yasio ya kuambukiza kama kisukari, shinikizo la damu na moyo. Kwa mtazamo wangu kuna kitu hakiko sawa na mamlaka ama hazisemi ukweli kwa sababu wanazozijua vizuri wao wenyewe au hazina maarifa ya kufanya uchunguzi usiofungamana na itifaki za kikoloni mamboleo za kufungwa na WHO.

Majibu mepesi yanayotolewa na wataalamu wetu wa afya na mamlaka husika kwamba matatizo haya yanatokana na kubadilisha staili za maisha kwa waathirika wa magonjwa haya ni uongo wa kitaaluma kuficha vyanzo halisi vya matatizo haya.

Mimi ni mfuatiliaji saana wa taarifa na habari ziitwazo conpiracy theories ambazo kwa hakika huletwa na ushahidi katika maandiko mengi sana. Moja wapo ni kua PHARMACEUTICAL INDUSTRY DOES NOT PRODUCE CURE BUT CREATES CUSTOMERS! Kwamba mabeberu hawa madawa ya binaadam na hata mifugo ni biashara yao kubwa na hawawezi kukubali kutokomeza kabisa magonjwa ulimwenguni kwa kuhofia kukosa fedha nyingi sana zilizopo kwenye magonjwa.

Jambo hili linaratibiwa kwa umakini mkubwa sana na mashirika ya kibeberu wenyewe tukiyaita ya Umoja Wa Mataifa kama vile WHO,FAO na mama yao UNDP! wanajua magonjwa kama Malaria na hata UKIMWI soon yatatoweka kwa kupata njanjo au tiba kabisa kwa hiyo ni bora kuja na kitu ambacho kitamfanya mgonjwa awe tegemezi na mteja wa dawa maisha yake yote! Watu wenye Kisukari na Pressure hushauriwa kutumia dawa miaka yote ya uhai wao hivo kua ni soko la uhakika sana la madawa haya. Soon utasikia malaria imetokomezwa ulimwenguni maana hailipi tena.

Ukichunguza kwa kawaida tu unga wa ngano kwa mfano tunaokula siku hizi upo tofauti sana na ngano tuliyokua tunatumia miaka ya nyuma. Hii ya siku hizi ambayo tunaambiwa imeongezwa 'virutubisho' vya lishe (ambayo ni miongoni mwa masharti yanayowekwa na watu kama FAO) ina matokeo ya kushangaza sana kwa walaji. Kwanza kwa watu wanaotumia unga huu wa ngano unaouzwa na makampuni makubwa kupikia chapati ama maandazi wajichunguze kama wanaweza kula sana products zake hizo(chapati na maandazi).

Miaka ya nyuma wakati tulikua tunakoboa na kusaga ngano halisi kutoka shambani sisi wenyewe na kupika vyakula hivo kuna watu walikua wanaondoka hata chapati kumi na humkuti na kitambi, kitu ambacho huwezi kuta kwa sasa. Sikuhizi watu wanakula chapati mbili au tatu lakini wanawake kwa wanaume wanashindana kwa vitambi! Na hii ipo katika vyakula vingi tunavyonunua kutoka makampuni makubwa
Mbaya zaidi kuna haya maji yanaitwa mineral water. Kutokana na kuonekana na kudhaniwa kua maji ya bomba hayako salama basi watu wote wamekimbilia kwenye maji ya chupa ya kununua yaliyo ongezewa kemikali viwandani. Kwa maoni yangu hili ni janga jingine ambapo ongezeko la matatizo ya figo linaloshuhudiwa kwa kasi ya kutisha huku makampuni ya kutibu maradhi haya(kiuhalisia hayatibu ila wanaukomaza tu ugonjwa na kutuliza hali) yakitengeneza faida kubwa sana(jaribu kuulizia gharama za kusafishwa figo katika mahospitali)

Japo wengi wetu(mimi nikiwemo) sio madaktari wala wataalam wa afya lakini athari na matokeo ya michezo hii tuinaipata moja kwa moja. Haya mashirika yanayoitwa ya Umoja Wa Mataifa sijawahi kuyaamini. Leo hii nchi yoyote duniani hasa ya dunia ya tatu ambao hawajui syndicate hizi igundue dawa ya kutibu maradhi ambayo ni tishio kwa watu wake basi kwa protocols za WHO huwezi tu kuanza kuwapa dawa hiyo watu wako bila idhini yake! Na kwa hila, utakapopitia kwao watau undermine ugunduzi wenu.

Ndio maana maradhi yoote ya kitropic yanapatikana katika nchi zinazoendelea(Nyerere aliwahi kusema haziendelei) dawa zoote zinatengenezwa na na makampuni machache ya Ulaya na Marekani na syndicates zao sehemu chache duniani!

Natamani nchi zetu zitengeneze espionage machinery kama hapa kwetu iwe chini ya TISS ili kujua ukweli kuhusu usalama wa afya za watu wake, vinginevyo pamoja na vikundi likuki vya jogging vinavyoanzishwa siku hizi baada ya kukaririshwa kua tunaumwa kwa sababu ya kubadilisha mfumo wa maisha, magonjwa haya ya kutengeneza yataendelea kumaliza watu wetu
 
Mkuu umemaliza kila kitu.Huko kwenye kilimo ni dawa tupu yaani kwa ufupi usipoinywa sumu utaila ata kwenye vyakula.Wulize wanaolima nyanya dawa zinazopigwa hukoo Sikiu izi mpaka kwenye mahindi.Wale wanaoikimbia soda wanabanwa kona nyingine hiyo inaitwa usipoinywa kwa soda utaila kwenye ugali.Kuna mmea mmoja unaitwa vinka kitaalamu uwa unatibu sukari na presha ila jamaa hawataki kusikia kazi yao kutuua na makopa yao.
 
Back
Top Bottom