Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
Kuna hoja ya kukaimu nafasi ya Jaji Mkuu.
Hoja hii imejadiliwa sana kabla Profesa Kabudi kuteulia kuwa Waziri wa Sheria na Katiba na bado inaendelea kujadiliwa . Kati ya watu walio jadili kwa urefu ni pamoja na Zitto Kabwe kwenye mkutano mkuu wao wa kidemokrasia.
Waziri wa Sheria na Katiba, akiwa kwenye kipindi cha maswali na majibu anasema si kweli kwamba nafasi hiyo haijawahi kukaimiwa baada mtangulizi wake kumaliza muda wake. Hayo yalikuwa majibu kwa Tundu Lissu ambaye ndiye msemaji mkuu wa kambi ya upinzani kwa mambo ya sheria na katiba. Katika hili alitolea mfano. Anasema baada yule Mwanasheria mkuu wa serikali ambaye alikuwa ni wa kiengereza kuondoka, Mwalimu Nyerere alimteuwa mwengine wa kukaimu. T. P. George kutoka Trinidad and Tobago ndiye aliyekaimu na kwa muda mrefu. Na ameeleza kwanini Mwalimu Nyerere amefanya hivyo na sababu moja kubwa ni kuwa hakukuwa na mtu mwenye sifa.
Hoja iliyopo inatokana na katiba ya sasa iwe ya 1977 au hivyo unavyotaka wewe ya 1985 baada kuandika tena upya. Kwa mfano hoja ya Zitto Kabwe kuwa kabla Jaji Mkuu kustaafu tayari inajulikana lini ataastafu kwa hiyo miaka miwili kabla unaweza kujuwa nani atashikilia nafasi hiyo. Jaji Mkuu kukaimu zaidi ya miezi mitano si bure kuna kitu na hapa nakubaliana na hoja ya Zitto Kabwe, kuwa Rais ameamua kufanya hivyo, iwe ni rahisi kumuondosha pindi akiona anaanza kwenda kinyume na matakwa yake.
Kwa hiyo, Profesa Kabudi lazima atumiee usomi wake kuifahamu dhana ya kukaimu. Huko nyuma iliwezekani mtu kukaimu kwa muda mrefu kwasababu hakukuwa na mtu mwenye sifa, hivi sasa yupo/wapo mwenye/wenye sifa.
Profesa Chode-chonde usije kugeuka Fracis Mutungi