Kuna heshima kubwa sana kuitwa Baba mjengo, jenga hata chumba kimoja

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Kuna heshima kubwa sana kuitwa Baba mjengo jenga hata chumba kimoja

Hivi kuna heshima kubwa kwa hapa mjini kama kuitwa baba mjengo?

Hakuna jambo lina faraja kama hilo, nimesema hili kwasababu nimeona kuna mtu nimeona anatangatanga huku na kule na mateso anayopata nyumba za kupanga

Nyumba za kupanga wakati mwingine ni utumwa huwa nashauri watu wakati mwingine wajenge hata chumba kimoja tu wahamie aweke kwanza kambi huku akiendelea kuchapa kazi na kuwaza kujenga nyumba ya ndoto yake mwishowe hicho chumba kimoja ulojenga na kukaa kwa muda unakuja kukipangishia wewe unakua ushajenga ya ndoto zako

Wengi wanatamani kujenga mjengo wa maana kwanza wakati kiwango hakitoshi, sikiliza kama unaona shida na nyumba za kupanga nunua kajikiwanja jenga kanyumba ka mchongo hata vyumba viwili au chumba kimoja hapo utakaa kusave hela za kulipa makodi kila mwezi na itaondoa stress za kulipa makodi kila mwezi pia hii itakupa mwanga wa kujidunduliza kujenga nyumba ya ndoto yako nyengine

Ila natoa indhari, kama unajenga hicho chumba kimoja km ni mbali na shughuli zako please usifanye hivyo endelea tu kubaki kwenye upangaji huku ukipambana

Ila kuwa mwenye nyumba raha sana
 
Naona mtu aangalie na consistency yake ya kupata pesa kwa mfano ana uwakika wa saving nzuri kutokana na kazi labda kwa kusave miaka minne au mitatu atakuwa labda na million 60 au zaidi basi anaweza kupanga kwa miaka hyo huku anajenga taratibu kikubwa asijinyime kwamba kujenga ndo akose hata akiba anaweza kuja kukopa bure...kusecure kiwanja ni muhimu hata kuweka msingi taratibu Kuna sehemu unakaa fresh sio lazima ujenge.

Kama pesa ni zile za dili umepata fasta unaweza kujenga hata vyumba viwili taratibu labda una mtoto mmoja mpaka wapili ukipata na huyu wa mwanzo akiwa mkubwa unakuwa uko mbali..
 
Back
Top Bottom