Kuna haja ya kubadili mfumo wa upigaji kura

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
11,495
24,212
Kwa aina hii ya wabunge tulionao wa pande zote nikimaanisha CCM na UKAWA kuna haja ya kubadili mfumo wa upigaji kura na wapiga kura kiujumla.Bila shaka sasa mtakubaliana na mimi kura ziwe zinapigwa na kundi fulani tu katika kila jimbo, kila jimbo linahitaji kuwa na watu wake wasiozidi 100 kupiga kura kwa niaba ya jimbo husika.

Lengo hapa ni kuzibiti nchi kuwa na wabunge wasioweza kulisaidia taifa au kuwakilisha vyema watu wao.Hawa watu wasiozidi 100 watakuwa wanatoka kwenye familia 100 tofauti zenye upeo na watu waliondelea kiuchumi,kidini na kiutamaduni katika jimbo husika.

Kuruhusu kila mtanzania kupiga kura kunaleta shida sana kwenye ngazi zote za ubunge mpaka urais. Kuna haja ya kuwa na jamii fulani kama wapiga kura kwenye jimbo husika ili kuondoa ujinga huu wakuwa na wawakilishi wasiokuwa na msaada kwa taifa.

Tujadili kumsaidia Mh. wetu labda ataweka hili kwenye katiba yetu.
 
Hata usisumbuke, hata wapige kura watu milioni saba, ila uamuzi wa mwisho unafanya na kamati kuu ya CCM, yenye wajumbe wasiofika 30.
 
Lakini angalau itasaidia kwa hii ngazi ya ubunge, udiwani, na uenyekiti kupata anagalau watu wenye upeo..
 
Kwa aina hii ya wabunge tulionao wa pande zote nikimaanisha CCM na UKAWA kuna haja ya kubadili mfumo wa upigaji kura na wapiga kura kiujumla.Bila shaka sasa mtakubaliana na mimi kura ziwe zinapigwa na kundi fulani tu katika kila jimbo, kila jimbo linahitaji kuwa na watu wake wasiozidi 100 kupiga kura kwa niaba ya jimbo husika.

Lengo hapa ni kuzibiti nchi kuwa na wabunge wasioweza kulisaidia taifa au kuwakilisha vyema watu wao.Hawa watu wasiozidi 100 watakuwa wanatoka kwenye familia 100 tofauti zenye upeo na watu waliondelea kiuchumi,kidini na kiutamaduni katika jimbo husika.

Kuruhusu kila mtanzania kupiga kura kunaleta shida sana kwenye ngazi zote za ubunge mpaka urais. Kuna haja ya kuwa na jamii fulani kama wapiga kura kwenye jimbo husika ili kuondoa ujinga huu wakuwa na wawakilishi wasiokuwa na msaada kwa taifa.

Tujadili kumsaidia Mh. wetu labda ataweka hili kwenye katiba yetu.
Ataliweka kwenye katiba ipi? Kwani kuna mchakato wa katiba unaendelea?
 
Kama anadhamira ya dhati ya kujenga misingi, anaweza kuvunja iliyopo na kuongeza hicho kifungu kikawa kama kiraka.
 
Back
Top Bottom