Nebuchadinezzer
JF-Expert Member
- Oct 1, 2018
- 1,403
- 2,545
Asalaam Walekum? Bwana Yesu apewe sifa? Mapendo? Mungu ni mwema? Maranatha? Natumaini kila mmoja wetu ni mzima wa afya? Kama sivyo, Mungu awafanyie wepesi mliowagonjwa na mlio katika shida mbalimbali.
Leo sina mengi sana ila naleta kwenu hoja yangu kama kichwa kinavyojieleza hapo juu.
Tangu nilipokuwa mtoto mpaka leo hii mimi ni mtu mzima ninayeweza kutengeneza watoto nimekua nikishuhudia mtu akifa anazikwa, wanaenda kumfukia chini ya ardhi, juu ya ile aridhi wanatengeneza kama msingi hivi na kuweka marumaru (vigae) halafu wanachomeka na msalaba wa mbao au wa chuma.
Badae nimekua na kwenda shule ambako nimefundishwa kutumia akili ya kiutafiti na kuhoji. Leo nimekaa zangu hapa nakula matunda akili ikanambia hakuna umuhimu wa kuzika.
Mimi naona kutokana na uhaba wa aridhi ni vizuri badala ya watu kuzikwa basi wakifa wachomwe moto tu. Wawe majivu halafu tuyamwage baharini au mashambani ili viumbe hai wengine kama mahindi wanufaike . Na pia tulio hai tufurahie maisha.
Mimi nadhani wafu wanachukua ardhi kubwa mno halafu hata hawaiendelezi. Zaidi ya hapo wanakua wanatutisha tu hata kupita maeneo yao usiku tunaogopa.
Halafu naamini wafu wakianza kuchomwa hata hizi imani zingine za kijinga kijinga za kuamini waliokufa na kuanza kuwajali na wakati kipindi wapo wazima tulikuwa tunawachukia zitaisha.
Si busara walio hai wakakosa ardhi halafu wafu wapewe.
Ni hayo tu jamani. Sina mengi leo. Mungu awabariki sana.
Hoja haipigwi rungu.