Kuna familia zimehukumiwa wasiolewe

Latifaa

JF-Expert Member
Jan 18, 2012
501
258
Ni kweli kuna familia nyingi zimehukumiwa wasiingie kwenye ndoa, hata wakiingia ndoa zao hazidumu wala kuwa na furaha na amani na hukumu hii siyo kwamba wamehukumiwa na Mungu lahasha wamehukumiwa na wachawi, na hili tatizo unakuta lilianzia mbali wakati mwingine.

Ushawahi kujiuliza ni kwanini watu fulani kwao kuolewa ni mbinde na hata akiolewa ndoa inakuwa migogoro migogoro yaani kama kulazimishana unakuta Dada mtu kaachika anafuatia hajaolewa, anaefuatia kaolewa ila ndoa ndoano na wenginewe.

Hivyo mtakaemuona ameolewa sio kwamba ana amani nae shida tupu ila uvumilivu wa haki ya juu. Wengine ambao hawajahukumiwa unakuta wanaolewa kirahisi na wanaume wema wanawapenda na kuwajali hawaachiki hata mwanamke awe kituko mumewe hamuachi na wadogo zake wanaolewa kirahisi kabisa yaani kuna familia unakuta watoto wote wameolewa na amani kwenye ndoa zao.

Unakuta mwanamke kimuonekano hana mvuto lakini mume wake anavyompenda na kumthamini hadi unastaajabu. Halafu unakuta mwingi ni mrembo kila idara ila mumewe Hana tyme nae mate so kwakwenda mbele hadi mnakosa jibu.

Issue kubwa hapo ni familia alimotokea wamehukumiwa nini? Kama mmehukumiwa msiolewe hata ungekua mrembo vipi ndoa kwako ni bure, kama hamjahukumiwa wewe mwanaume kwako ni amani na upendo hata kwenye mahusiano unapata mahusiano yenye furaha.

Natoa ushauri ewe dada jichunguze je familia yenu imehukumiwa kutokuolewa jinsi yakujua nikuyaangalia mahusiano yako na kama umeshaolewa ndoa yako ikoje na ndugu zako wakoje na ndani pia wakoje? Ukishapata jibu fanyia kazi jibulako.
 
Sasa ungewashauri hao waliohukumiwa wafanyeje ili wakate rufaa, maana hukumu zingine ni za uonevu kabisaa kwa makosa ambayo hawajayafanya
Ukishajigundua uko kundi lipi ndio uchukukuea hatua
 
Hio kitu ipo nimeishuhudia kwa macho yangu.

Kuna jirani yangu huku uswahilini ana mabinti wanne na vijana wa kiume watatu.
Wote wakiolewa wanaishia kuachika tu na kurudi nyumbani na vijana pia wakioa wanawake wanawakimbia.

Ukifuatilia stori ya hio familia unakuta mama mtu mzaa hao watoto naye aliolewa lakini mwanaume kamkibia na kuna tetesi pia hata bibi ambaye ndiye mama wa huyo mama ambaye watoto wake hawaolewi wala kuoa naye aliolewa akaachika na kubaki hivyo hivyo bila mume.

Taarifa za chini chini zinasema kuwa chanzo ni mambo ya kishirikina kwani familia hiyo huko kwao wanaendekeza sana mambo ya uchawi na hio kutooa au kuolewa ni moja ya agano waliloingia na vilinge vyao ili kupata nguvu za uchawi.

Hio siri wanaijua wachache sana katika familia yao, hasa watu wazima, watoto na wajukuu hawajui na wanateseka sana kwa kuachika na kuachwa.
 
Back
Top Bottom