Kuna familia kweli hapa mjini DSM hawajui makande?

ommytk

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
482
1,053
Wadau nimeona hili niwape huku na ninyi mpate kushangaa kama Mimi.

Leo tulipata ugeni nyumbani kuna rafiki yangu jirani yangu anakaa Masaki alinipigia simu nimtafutie kiwanja huku Kigamboni nikapambana nikapata.

Leo amekuja kukagua sasa kaja na wanae wawili mmoja miaka 16 mwingine kama 9 hivi, baada kukagua wamekipenda kesho ataenda benki kulipia sasa muda ukawa umefika wa chakula cha mchana.

Tumepita home apajue tukakuta Dada ameandaa lunch nikawaribisha ndani basi tukaanza kupakua chakula, wale watoto wanaongea kizungu mie sikujua lakini baba yao ndio akaniambia aisee hawa madogo awali ngoja nipige Mimi hizi kande chap chap (ni chakula mahindi wanachanganya na maharage).

Basi ikabidi tuwatafutie soda jamaa akasema hicho chakula hawakijui na wala hawajawahi kukiona aiseee nikasema kuna watu wanaishi aisee kumbe kuna nyumba hazijui kande.
 
Baada ya miaka kubalehe, hao watoto ndo utasikia nguvu za kiume kalas!
Bora wangesema ata wameshiba vijana wape juisi tu au maji wametoka kunywa vhai muda tu so mrefu kuliko kusema iki chakula awakijui
 
Cha ajabu nini hapo?
Wazazi wamezaliwa DSM, watoto kazaliwa DSM, kakulia DSM, anasoma DSM hata boarding hajui.
Sasa makande atapishana nayo barabara gani?
Makande tunakula nyumbani sio boarding, la sivyo Wapare wote wako boarding!
Ni malezi ya hovyo, kuna ambaye amezaliwa na kujua kila aina ya chakula? Si unaonja kidogo. Hata wazungu wanaofikiri ndio wanawaiga hawako hivyo.
 
Makande tunakula nyumbani sio boarding, la sivyo Wapare wote wako boarding!
Ni malezi ya hovyo, kuna ambaye amezaliwa na kujua kila aina ya chakula? Si unaonja kidogo. Hata wazungu wanaofikiri ndio wanawaiga hawako hivyo.
Mkuu wewe pengine umesoma boarding za St Mzungu!

Siye boarding za Kayumba hicho chakula kawaida sana na kitamu tu.

Hata kule Kenya kinaliwa sana boarding, kinaitwa mudhokoi.
 
Wadau nimeona hili niwape uku nanyonyi mpate kushamgaa kama Mimi Leo tulipata ugeni nyumbani kuna rafiki yangu jirani yangu anakaa masaki alinipigia simu nimtafutie kiwanja uku kigamboni nikapambana nikapata Leo amekuja kukagua sasa kaja na wanae wawili mmoja miaka 16 mwingine...
Kutokujua chakula haina maana huwezi kujaribu kukila. There is always a first time for everything. Halafu kutokula makande hakuna connection na pesa wala nini. Mfano hata mimi kwangu hakujawahi kupikwa makande na siyo kwamba ni tajiri wala makande ni chakula cha maskini, ni kwamba ni chakula ambacho sikipendi na huenda mwanangu hajawahi kula makande kama kayala basi siyo hapa nyumbani.
 
Sio tu wa Ushuani hata sisi wa bush kande tumekuja kulionea shuleni, jamii yetu mtu alikuwa akipika kande anasikitikiwa kwamba kaishiwa.
Ni kweli kabisa mkuu, hata mimi kande nimekuja kulila nikiwa boarding advance. Sikuwahi kula kande hapo kabla na hii haimanishi kuwa ni ushua wala nini, jamii yetu kande siyo chakula chetu kabisa.
 
Wadau nimeona hili niwape uku nanyonyi mpate kushamgaa kama Mimi Leo tulipata ugeni nyumbani kuna rafiki yangu jirani yangu anakaa masaki alinipigia simu nimtafutie kiwanja uku kigamboni nikapambana nikapata Leo amekuja kukagua sasa kaja na wanae wawili mmoja miaka 16 mwingine kama 9 hivi baada kukagua wamekipenda kesho ataenda bank kulipia sasa muda ukawa umefika was chakula cha mchana tumepita home apajue tukakuta Dada ameandaa lunch nikawaribisha ndani basi tukaanza kupakua chakula wale watoto wanaongea kizungu mie sikikujua lakini baba yao ndio akaniambia aisee awa madogo awali ngoja nipige Mimi hizi kande chap chap (ni chakula mahindi wanachanganya na maharage)basi ikabidi tuwatafutie soda jamaa akasema iko chakula awakijui na wala awajawahi kukiona aiseee nikasema kuna watu wanaishi aiseeeeee kumbe kuna nyumba azijui kande aiseeee
Mkuu wewe ushawahi kula buttermilk rusk au Corn Flex? bora unawanunulie wale au jipinde uwapikie Chicken Flied rice...

Usimlishe mgeni wako chakula unachopenda wewe bora uulize utakuja lisha Waislam Mbuzi katoliki
 
Ni kweli kabisa mkuu, hata mimi kande nimekuja kulila nikiwa boarding advance. Sikuwahi kula kande hapo kabla na hii haimanishi kuwa ni ushua wala nini, jamii yetu kande siyo chakula chetu kabisa.
Msio wakulima makande kwenu ni tabu kbisa kuna aina na aina za makande
Kande za maziwa
Kande za mahindi mabichi(tamu sana hata unaweza kuvimbiwa)
Kande za siagi(za siku hizi)
Kande za msibani(mahindi na harage makavu)
n.k. n.k.

Kande ni chakula all round,
 
Msio wakulima makande kwenu ni tabu kbisa kuna aina na aina za makande
Kande za maziwa
Kande za mahindi mabichi(tamu sana hata unaweza kuvimbiwa)
Kande za siagi(za siku hizi)
Kande za msibani(mahindi na harage makavu)
n.k. n.k.

Kande ni chakula all round,
Kuna kande nilikula kwa wacameroon, ni kande limechanganya maharage, mahindi na samaki wale wale smoked, pilipili, na mammbo mengine sijui. Lilikuwa tamu balaa yani lilikuwa kande mojja matata ndilo kande nililowahi kupenda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom