Kuna dawa ya kuondoa hamu ya kula?

vaati

Member
Jul 12, 2016
31
7
Habarini wadau, Shikamooni wakubwa

Naombeni ushauri kwenu kuhusu hili tatizo langu. Mwenzenu napenda kula kupita maelezo, sasa hili tatizo linaniboa pia linanisikitisha kiafya. Maana sometimes nakuwa mvivu nikishiba sana.

Napenda nile kidogo ila nashindwa na hili tatizo limenisababishia kuwa na tumbo kubwa ambalo nalichukia. Nisaidieni kwa mawazo.
 
Anza kupunguza kidogo kidogo, kama ilikua unakula maandazi 10 anza kula 8, baadae 6 hadi ufike mawili, mwili ukiuzoesha kula kidogo unakubali
 
...anza kula chakula usichokipenda, naamini utakula kidogo tu lkn ukiendekiendelea kula chakula unachokipenda utaendelea kula sana...
 
dawa ya kupunguza kula hakuna ila dawa ya minyoo ipo

tafuta dawa ya minyoo utafune au kazi unazofanya zinakufanya ule sana au mazoezi yanachangia ule sana la sivyo huli peke yako upo na minyoo
 
Habarini wadau,
Shikamooni wakubw,,
Naombeni ushauri kwenu kuhusu hili tatizo langu,mwenzenu napenda kula kupita maelezo sasa hili tatizo linaniboa pia linanisikitisha ki afya....maanake sometimes nakua mvivu nikishiba sana .....napenda nile kidogo ila nashindwa na hili tatizo limenisababishia kuw na tumbo kubwa ambalo nalichukia.....nisaidieni kwa mawazo.

Kama unatumia dawa za minyoo vizuri na bado hali iko pale pale basi uwe unakula vitu vidogo vidogo visivyo na mafuta mara kwa mara na kunywa maji mengi ya kawaida sio toka frijini kabla ya kula mlo mzito kama chakula cha mchana au usiku
 
anza kupunguza kipimo cha kula kwa mfano asubuhi unakunywa uji kikombe kimoja bila kitafunwa na hakikisha mwili wako unajishulisha kufanya mazoezi ya viungo mpaka unatoa jasho ndani ya siku saba utakua umepunguza kiwango cha kula na jiwekee ratiba maalumu ya kula walau kwa siku mara tatu
 
dawa ya kupunguza kula hakuna ila dawa ya minyoo ipo

tafuta dawa ya minyoo utafune au kazi unazofanya zinakufanya ule sana au mazoezi yanachangia ule sana la sivyo huli peke yako upo na minyoo
Nimeshatavuna hata mwezi bado mkuu ....ila bado nakamua msosi
 
Kama unatumia dawa za minyoo vizuri na bado hali iko pale pale basi uwe unakula vitu vidogo vidogo visivyo na mafuta mara kwa mara na kunywa maji mengi ya kawaida sio toka frijini kabla ya kula mlo mzito kama chakula cha mchana au usiku
Asante...
 
anza kupunguza kipimo cha kula kwa mfano asubuhi unakunywa uji kikombe kimoja bila kitafunwa na hakikisha mwili wako unajishulisha kufanya mazoezi ya viungo mpaka unatoa jasho ndani ya siku saba utakua umepunguza kiwango cha kula na jiwekee ratiba maalumu ya kula walau kwa siku mara tatu
Thanks darling
 
hili tatizo hata mimi nlikua nalo ila baada ya kuanza kujipikia mwenyewe nikashangaa nmepona gafla,njaa ikiniuma nikitaka kufanya mambo yangu mara vyombo hivi hapa vichafu .hamu yote inaisha nanunua chips navunga
 
Back
Top Bottom